Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Nchi hii tusioamini hayo mambo ya kichawi twaweza tusifike hata watu 100!
Humu JF yenyewe tu sidhani tunafika hata watu 6!
Wengine wote waliobaki ni watu wenye kuamini hayo mambo, ambayo kiuhalisia hayapo.
Uchawi haupo. Ni fiksi tu. Ni uongo ulio mrahisi kuugundua.
Kitendo cha binti mrembo mwenye ulemavu wa ngozi kunyakuliwa na watu halafu wakaenda kumuua na kumnyofoa baadhi ya viungo vyake vya mwili, kimeumiza watu wengi sana.
Hakuna sababu ingine ambayo inaweza kuwa ndo sababu ya kumfanyia unyama huo zaidi ya mambo ya kishirikina.
Hii si mara ya kwanza kwa mtu mwenye ulemavu wa ngozi kukutwa na dhahma ya namna hiyo.
Tanzania matendo hayo kwa hao watu yamekuwa ni ya kawaida [licha ya kwamba hayakubaliki hata kidogo].
Hivyo, hili tukio la binti mrembo si la kwanza na halitokuwa la mwisho kutokea.
Na pengine yapo matukio mengine kama hayo ambayo hayapati tu uenezi.
Naunga mkono wahusika wote wa matukio kama hayo kuadhibiwa kwa kiwango cha juu kabisa kinachoruhusiwa kisheria.
Na ingekuwa ni juu yangu kuwaadhibu wakosaji, baada kuthibitisha pasipo na shaka kuwa wanahusika moja kwa moja, sheria ningeiweka kando na kuwapa adhabu wanayoistahili!
Lakini kwenye jamii ambayo imani za kishirikina zina mizizi mirefu, ukiondoa sisi wachache ambao hatuamini kabisa hayo mambo, ni nani wa kuzikemea hizo imani potofu na kutoa elimu ya kuufuta huo ujinga?
Manake watu ambao mtu ungedhani kuwa labda ndo wanaweza kuongoza kutoa elimu na kuufuta huo ujinga, ndo wanaongoza kwenye kuziamini hizo imani potofu.
Bila kuondokana na hizo imani, matukio ya mauaji ya albino yataendelea kutokea.
Rais, ambaye ana bully pulpit ya urais, wala humsikii akiongoza kuelimisha watu kwamba uchawi au hizo imani za kichawi, ni fiksi tu.
Viongozi walio chini yake nao hamna kitu.
Hayo yote ni ishara ya kwamba hata wao wanayaamini hayo mambo licha ya fursa za kielimu na za kiufunuo walizo nazo.
Biła ya kuachana na hizo imani, hayo matukio ya namna hiyo yataendelea kutokea.
Kifo cha binti kimenisikitisha sana. Natamani ningekuwepo wakati wameenda kumnyakua maana nina uhakika binti angelikuwa yu hai leo hii.
Kitendo kama hicho hakiwezi kutokea mbele yangu halafu pasiwe na consequences kwa hao wahalifu.
I hate the emfers who took her life with passion.
I wish I would……
Pia soma:
- Update: Mwili wa Mtoto Albino (Asimwe) wakutwa hauna baadhi ya viungo
- Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualbino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchungu
- Kufuta mauaji ya albino, ni kutokomeza kabisa Waganga wapiga ramli