Nani wakuangaliwa zaidi?

Nyundo_tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
640
Reaction score
20
Kumekuwa na kasumba hapa nchini kwetu ya kuwakaribisha kwa bashasha esp kwa watu walioweza kufanya mambo fulani makubwa. Hilo sikatai lakini jeh, kuna haja ya kufanya zaidi ya hapo? Kwa mfano, hivi majuzi Hashim Thabeet (kijana aliyetumia juhudi zake binafsi kufika hapo alipofika), alirudi nchini na kupokelewa na viongozi wa serikali na si kwamba hiyo ilitosha bali pia alipata fursa ya kukaribishwa ikulu. Lakini je! Na wale wasiojiweza kama vile ombaomba, wajane, watoto wa mitaani n.k walishawahi fanyiwa hivyo?. Ikumbukwe hawa Wako hapa hapa nchini….!

Nani wakuangaliwa zaidi? Waliofanikiwa tayari, au hawa waliochini? NISAIDIENI WADAU…
 
Utaumiza kichwa bure na taratibu na tabia za watu dunia hii, si Tz tu, inabidi individuals wabadilike

Umeshawahi kuwakaribisha hao vilema n.k ngau hata kuwapa chochote !

Kama hujafanya, tukikupa urais you will be as THEM!
 

Simple... where do you focus for your development juu au chini??? that being said kila mmoja na nafasi yake, maskini na mlemavu pia ana nafasi yake katika jamii, wewe hukumbuki Mengi pia huwaalika na kula nao pamoja?? Je wewe ukirudi kule kijijini unatumia muda mwingi na nani? na ukiwa mjini do you spend the same proportion amount of time na walio juu au chini??

Depending on how you perceive, kila mmoja ni wa kuangaliwa zaidi kwa nafasi yake
 
Mzee Mwinyi alianza na Huu utaratibu wa Kukutana na wananchi kueleza shida zao face to face...!!! Ilisaidia sana...!!!

Kimsingi GOT inatakiwa kuwaangalia wananchi wote kulingana na mahitaji anuai
 

Huoni kwamba anahitaji makaribisho hayo kwa jinsi alivyojituma?
 

Issue kwamba Thabeet amefika hapo alipo kwa juhudi zake binafsi sio la msingi. La msingi ni kwamba pamoja na juhudi zake hizo, ambazo zinafaa kuigwa na kila mtu katika nyaja yeyote mtu huyo alipo, Thabeet ameletea Taifa la Tanzania sifa. Hii ndio sababu amepokelewa na viongozi wa serikali na wananchi wa Tanzania, namna hiyo. Atakapokuwa akicheza ligi ya NBA ikianza, bendera ya Tanzania, Marekani na nchi nyingine ambazo wachezaji watakuwa wanatoka zitakuwa zinapepea kwenye arena yeyote ile timu yake itakapokuwa ikicheza hapa na hiyo si sifa kwa Thabeet tu bali na Tanzania kwa ujumla.
 
Hasheem akiamua kuchukua uraia wa Marekani naona 'DC' itapitishwa haraka sana na Waheshimiwa ili 'tusimpoteze' Mtanzania mwenzetu. Kwa maoni yangu HT alistahili mapokezi aliyoyapata maana mpaka sasa hivi amekuwa balozi mzuri sana wa nchi yetu.
 
Yah! Nimekubali waheshimiwa na maoni yenu ya msingi... Nilichokuwa naomba ni atlist siku moja mzee Bendera awaite na wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…