Nani yu nyuma ya mgogoro wa mpaka Tanzania VS Malawi?

Nani yu nyuma ya mgogoro wa mpaka Tanzania VS Malawi?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
Awali, Tanzania na Malawi walikubaliana kutatua mgogoro huu kwa kutumia njia ya mazungumzo ya pande mbili ambapo walikubaliana kutafuta washuluhishi wanaokubalika na Pande zote mbili. Wasuluhishi waliokuwa wamekubalika kwamba wasaidie kwenye kutatua mgogoro huu walikuwa ni marais wastahafu wa Nchi za SADC wakiongozwa na Rais wa zamani wa Msumbiji; Ndugu Joachim Chissano.Licha ya kuwa uamuzi huu ulikuwa ni mzuri kwa kuwa mazungumzo ndio njia bora kabisa ya utatuzi wa migogoro, Malawi iliripotiwa na baadhi ya wachambuzi wa mambo kutoridhishwa na njia hii na kukubali kwa shingo upande.Sasa jambo la kusikitisha ni kwamba Rais wa Malawi Bi. Joyce Banda ameamua kujitoa kwenye mazungumzo maskini!
"Malawi turns to courts over Tanzania dispute"

Wednesday, 03 April 2013 00:00

"LILONGWE. — President Joyce Banda has said that Malawi was giving up on mediation efforts and would take to the courts to settle a long-dormant border dispute with Tanzania, which has been re-activated by prospects of an oil find.

“Our view is that we should eventually go to court. We should not waste time on this (mediation),” Banda told reporters in Lilongwe on Monday after returning from visits to the US and Britain.

She said the mediation bid left to Mozambique’s ex-president Joaquim Chissano in his capacity as ahead of a forum of retired leaders from the regional bloc Sadc, was “compromised because information submitted by Malawi was leaked to Tanzania”.

She accused the executive secretary of the forum, John Tesha, a Tanzanian national, for leaking some vital information to his home country.

“After surrendering our documents, we were told that they were leaked to Tanzania before the Tanzanians surrendered theirs,” Banda said.

“We feel everything is compromised,” she said. In December Banda said the dispute had dragged for too long and she was considering taking it to the International Court of Justice for arbitration.

At stake is a largely undeveloped swathe of the lake where Malawi has awarded a licence to British firm Surestream to explore for oil in the north-eastern waters near Tanzania.

Malawi claims ownership of the entire lake under an 1890 agreement, while Tanzania disputes this validity, insisting part of the lake falls within its borders.

Talks in the past ended in a deadlock"
Wameripoti "Pan-African News wire" jana.
Alipokuwa akihojiwa na BBC jana, Msemaji wa Tanzania alisema Licha ya kwamba wamesikitishwa na taarifa hiyo, ni jambo wallilokuwa wanalitegemea kwa kuwa Malawi walionekana kupinga njia ya mazungumzo kama njia bora ya usuluhishi.Hata hivyo alisema Malawi haina uwezo wa kuishitaki Tanzania kwenye mahakama ya Kimataifa, bali Tanzania ndio wenye uwezo wa kufanya hivyo kwa kuwa kuna vigezo ambavyo Malawi hawajatimiza kwenye mahakama hiyo.

My take;
Binafsi napata mashaka kwamba kuna watu wako nyuma ya mgogoro huu na lengo lao kuu ni kuhakikisha wanafanya kila wawezalo kuhakikisha usuluhishi wa kidiplomasia haufui dafu.Pengine lengo lao ni kupata tenda ya kuuza silaha na viungo vya bandia. Hata hivyo nikijaribu kutafiti nashindwa kujua ni nani hasa lakini haiingii akilini usuluhishi kukwama kwama namna hii bila sababu za msingi.Sijui ninyi wenzangu mnaona je?

 
Kwanza naamini wakubwa hususan UK na US ndo wanaweza kuwa nyuma ya suala hili kwa kuzingatia kuwa kampuni tajwa ni ya UK.

Kwa upande mwingine inawezekana chokochoko hizi zikaathiri uwekezaji katika Mtwara Corridor? Inawezekana ikawa ni bora kuendeleza bandari ya Bagamoyo kama inavyokusudiwa kuliko kuendeleza ukanda ambao twaangaliana na jirani kwa jicho la husuda?
 
ubabe wetu huenda ndion unaowasukuma malawi ku re act the way wana react. Msikilize Lowasa alivyoanza.. msikilize Membe anavyo kuwa mkali.. Msikilize Kikwete alivyolizungumzia tatizo hilo mwaka jana.. katika hali kama hii inabidi busarara na hekima zitawale kuliko vitisho.. wenzetumalawi wana kila evidence mkononi sisi hatuna au tunayo!! Ramani zetu tunachora wenyewe je zimekubalika kimataifa..Tujifunze diplomasia
 
Huyo mmama Joyce Banda anajiamini sana kupita kiasi sio bure nyuma yake yawezekana kuna mkono wa mtu hasa mataifa yanayomendea rasilimali zetu,wakiona tunazielekeza rasilimali zetu china tena kwa mikataba mingi na ya muda mrefu watatumia njia za kuibua migogoro hata kufikia kupigana Nchi na Nchi ili wao watuuzie silaha na wajichotee kila wakitakacho bila ya bughudha.
 
Jambo lilowazi ni kwamba statement ya kujitoa kwenye mazungumzo ya upatanishi aliyatoa baada ya kurudi kutoka ziara ya Uingereza na Marekani. Kwa hiyo ukweli ni kwamba walio nyuma ya ili ni waingereza kwani kampuni inayofanya utafiti ni ya huko.
 
Jambo lilowazi ni kwamba statement ya kujitoa kwenye mazungumzo ya upatanishi aliyatoa baada ya kurudi kutoka ziara ya Uingereza na Marekani. Kwa hiyo ukweli ni kwamba walio nyuma ya ili ni waingereza kwani kampuni inayofanya utafiti ni ya huko.
Sasa kama ndio hivyo; sisi tunachotakiwa kufanya ni nini? Je! tunatakiwa tuwawashie moto Uingereza!
 
Wakuu! Binafsi naamini kuwa Uingereza ipo nyuma ya sakata hili. Hata ukiangalia juhudi inazofanya kujaribu kurejesha amani nchini Somalia (rejea mkutano mkubwa ulioitishwa na Bw. Cameroon kuhusu amani ya Somalia) utabaini kuwa Uingereza imejipanga kuhodhi raslimali hasa Gesi asilia na Mafuta ktk ukanda huu wote, kuanzia bahari ya Hindi mpaka eneo lote la maziwa makuu.

Tayari Uingereza inaendesha miradi karibia yote ya utafutaji na uchimbaji hasa wa Gesi asilia ktk pwani yote kuanzia Pwani ya Mocambique mpaka pwani ya Kenya. Na sasa wanataka Somalia itulie japo kiduchu wapate watakacho.
 
Niliwahi kupata taarifa kuwa Malawi wanajiandaa kuchimba madini ya urani (Uranium). Wamefikia hatua gani?
Kwa upande wetu, kampuni inayochimba (Namtumbo au Mkuju?) ni ya Urusi?
 
Hili jambo inabidi ulitazame kwa jicho la tatu waingereza walipopewa idhamini na umoja wa mataifa kututawala hadi tutakapokuwa kuwa tayari ukiangalia huyo ndio aliingia mkataba wa matumizi ya ziwa victoria viongozi wetu inabidi wawe na ujasiri wa kuwaambia hatutambui mikataba yote iliyoingiwa wakatu tuko chini yao lakini kukosa kwetu ujasili ndio kunawapa viburi
 
Kuna taarifa zinasema kuwa Malawi imeridhia mazungumzo yaanze kama awali.

Hata hivyo dada Joy, umaarufu wake unaendelea kushuka kutokana na siasa zake za mrengo usio eleweka (tofauti na watangulizi wake) hii ni kulingana na gazeti la Nyasa Times.

Inawezekana hizi zote ni kash-kash zake kuelekea uchaguzi wa Urais unaotarajiwa hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom