Nani yupo nyuma katika matukio haya ya Tindikali?

Nani yupo nyuma katika matukio haya ya Tindikali?

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,742
Ndugu wana JF tumeshuhudia matukio ya Umwagiwaji wa Tindikali kwa watanzania wenzetu na sasa imevuka mipaka hadi kwa raia wa Kigeni. Tukiorodhesha matukio ni mengi miongoni mwa matukio ni kama haya yafuatayo

1. SAID KUBENEA (2008) – Tanzania Bara
Kubenea.JPG
SMS Zifuatazo alitumiwa Kubenea kabla ya kukutwa na unyama ule.
Kubenea, news editor with Kiswahili weeklies, Mwana Halisi and Mseto has come out fearlessly last year to expose scandals, office abuse and allegations of embezzlement of public funds involving big shots within and outside the government.

He vowed, however, at his bed not to give up with investigative journalism that has increasingly put his life in jeopardy in recent months.

The writer has received at least 15 text messages from unknown persons from June last year threatening to terminate his life shouldn't he stop following up their life.

"Your death will be of its kind that your body will never be found," one of the SMS he received read.

Another reads:" Take your last breath. We are not far from you. Few hours are left before we send you where you deserve."
"Watch out we are not joking on this. We want your death to be a threat even to mabwana zako.
Tumeona SMS hizo lakini hakuna aliyekamatwa
2. Mkurugenzi wa Manispaa Zanzibar (Rahid Ally Juma) 2011 - Zanzibar
3. Musa Tesha – Igunga 2011 – Tanzania Bara
4. Shehk fadhir Suleiman – Zanzibar – Nov. 2012 - Zanzibar
5. Mohamed Kidevu – Sheha wa Tomondo Zanzibar – May 2013 - Zanzibar
Tindikali - Sheha wa Tomondo Mohamed Kidevu Zanzibar.jpg
6. Said Makamba – Shehk Wilaya ya Arumeru – July 2013 – Tanzania Bara
Tindikali Shehk Arumeru.png
7. Said Mohamed Saad Mmiliki wa Home Shopping center – Tanzania Bara
Lengo halisi la kuandika haya ni kutokana na tukio la jana lililosababisha Shehk Ponda kupigwa risasi kwani vyombo vya kimataifa vililiingiza tukio lile kwamba shehk ponda amepigwa risasi na kukamatwa na polisi kwa sababu ya kuhusika kwake katika kumwagiwa Tindikali wale Mabinti wawili wa Uingereza. Nimepata wasiwasi kwani inawezekana kabisa kilichofanyika ni kutaka Serikali kujiosha mbele ya jumuia za kimataifa kwa kuonyesha ni wafuatiliaji wa Karibu na wapo makini kufuatilia uhalifu kwa kumuingiza Shehk Ponda na tukio lile kama walivyozoea kubambikia watu kesi na lengo nafikiri ilikuwa ni kumuua na ili yeye kama yeye ndo asimame kama mtuhumiwa wa sakata lile la tindikali kwa Raia wale na mchezo ndiyo uwe umeishia hapo.
Katika mlolongo wa waliomwagiwa Tindikali kuna mashehk watatu wawili Zanzibar na mmoja Tanzania Bara lakini hatujasikia juhudi zozote za kina zinazoonyesha kutafutwa waliofanya uhalifu huo nah ii kuonyesha udhaifu mkubwa kwa vyombo vyetu vya usalama,
Tukio la Polisi na Serikali kumuingiza Shehk Ponda na tukio lile la kumwagiwa Tindikali wale Mabinti ni kitu kilichopangwa kwani tulimsikia DPP akitamka kuwa tukio lile sio la Ugaidi na bila kutoa ufafanuzi ni tukio la aina gani kwa hiyo jibu lake limepatikana hapo jana KUWA TUKIO LILE NI LA KIDINI na tusipoangali hawa viongozi wetu wanaweza kutuingiza katika mgawanyiko mkubwa wa kidini kutokana na kauli zao na matendo yao ni vizuri wakawa wanatafakari mambo kabla ya kuchukua uamuzi kwanza.
NAWASILISHA.
 
Nani yupo nyuma katika matukio haya ya tindikali?

"HATA MIMI SIJUI...."
 
vyombo vya dola ndo vinatakiwa vijibu mambo hayo........... failures za vyombo vya dola au vyombo vya dola kuweka priority katika mambo yasiyo ya msingi matokeo yake ndio haya!!!!!!!!!!! vyombo vya dola vinaitaj major overhaul!!!!!!
 
Sheikh Ponda huwa muwazi katika harakati zake. Huwa hashambulii imani nyingine. Yeye huishambulia serikali kwa kukandamiza haki na madai ya Waislamu. Amekua akilalamikia mkataba kati ya serikali na makanisa (mou) wa mwaka 1992, upendeleo wa Baraza La Mitihani la Taifa kwa imani za Kikristu dhidi ya watahiniwa Waislamu, uuzaji holela wa mali za Waislamu unaofanywa na BAKWATA, kufungwa kwa Masheikh na kuwazuia magerezani bila ya kosa linalo eleweka pamoja na kunyimwa dhamana, Waislamu kunyimwa haki ya kuwa na Mahakama ya Kadhi, na hivi majuzi alilaani uwepo wa kamati za ulinzi misikitini ambazo zinakua chini ya ocd. Maimamu na Masheikh watalazimika kupeleka hotuba za siku ya ijumaa kwenye kamati hizo kabla hazijasomwa kwa waumini.

Sheikh Ponda hajawahi kuhamasisha Waislamu kuwashambulia waumini wa dini nyingine. Vile Waingereza wameshambuliwa Zanzibar, serikali inamtumia Ponda kama kafara ili kuwafurahisha Wazungu. Alikwenda Zanzibar na kufanya mhadhara akilaani Masheikh wa Uamsho kuzuiliwa bila kupewa dhamana.

Serikali imesahau kuwa Ponda ana ushawishi mkubwa kwa Waislamu. Kitendo cha kumdhuru au kumuua, kinaweza kusababisha amani kutoeka nchini kwa kiasi kikubwa.
 
Hakuna upendeleo wowote pale NECTA. husomi hufaulu, period

Sheikh Ponda hajawahi kuhamasisha Waislamu kuwashambulia waumini wa dini nyingine. Vile Waingereza wameshambuliwa Zanzibar, serikali inamtumia Ponda kama kafara ili kuwafurahisha Wazungu. Alikwenda Zanzibar na kufanya mhadhara akilaani Masheikh wa Uamsho kuzuiliwa bila kupewa dhamana.

Serikali imesahau kuwa Ponda ana ushawishi mkubwa kwa Waislamu. Kitendo cha kumdhuru au kumuua, kinaweza kusababisha amani kutoeka nchini kwa kiasi kikubwa.
Kwenye blue, Rais JK amekwisha itolea ufafanuzi ulio wazi, lakini yeye
hataki kukubali. Hata wewe kwa akili yako unaweza leo kukubali kua
serikali iondoe ruzuku pale Bugando MC au iondoe ruzuku pale KCMC,
hospital za Ndanda, Sikonge, Kilangala, Mahenge, Ifakara. Kisa kumtii
Shk. Ponda. Basi hiyo serikali itakuwa haiwapendi kabisa wananchi wake,
na death toll itakuwa kubwa sana. Wote wenye akili wanajua umuhimu
wa hiyo ruzuku kwa taasisi hizo

Mahakama za kadhi zipo na zinaendeshwa na Waislam wenyewe,
ila yeye anataka ziendeshwe na serikali. Wakati serikali yetu sio
mali ya dini fulani.

Kuhusu uuzaji wa mali za Waislam, tayari imethibitika mahakamani
kuwa he is wrong, ndiyo maana mpaka yuko kifungoni mwaka mmoja,
kifungo cha nje. Huyo jamaa ana lake jambo, kwanini baada ya muda
mfupi baada kuwa kwa wazenj, acid attacks zimetokea, nini aliongea
nyuma ya pazia, is the question todebate.
 
Sheikh Ponda huwa muwazi katika harakati zake. Huwa hashambulii imani nyingine. Yeye huishambulia serikali kwa kukandamiza haki na madai ya Waislamu. Amekua akilalamikia mkataba kati ya serikali na makanisa (mou) wa mwaka 1992, upendeleo wa Baraza La Mitihani la Taifa kwa imani za Kikristu dhidi ya watahiniwa Waislamu, uuzaji holela wa mali za Waislamu unaofanywa na BAKWATA, kufungwa kwa Masheikh na kuwazuia magerezani bila ya kosa linalo eleweka pamoja na kunyimwa dhamana, Waislamu kunyimwa haki ya kuwa na Mahakama ya Kadhi, na hivi majuzi alilaani uwepo wa kamati za ulinzi misikitini ambazo zinakua chini ya ocd. Maimamu na Masheikh watalazimika kupeleka hotuba za siku ya ijumaa kwenye kamati hizo kabla hazijasomwa kwa waumini.

Sheikh Ponda hajawahi kuhamasisha Waislamu kuwashambulia waumini wa dini nyingine. Vile Waingereza wameshambuliwa Zanzibar, serikali inamtumia Ponda kama kafara ili kuwafurahisha Wazungu. Alikwenda Zanzibar na kufanya mhadhara akilaani Masheikh wa Uamsho kuzuiliwa bila kupewa dhamana.

Serikali imesahau kuwa Ponda ana ushawishi mkubwa kwa Waislamu. Kitendo cha kumdhuru au kumuua, kinaweza kusababisha amani kutoeka nchini kwa kiasi kikubwa.
penye red->umesema mengi, na mengine yamejaa hisia tu(penye blue).
(namna nyingine ya hisia ni kama kusema hivi.., shekh anataka kuwafurahisha waarabu kwa kuwamwagia wazungu tindikali)
j
e ninani anafanya jambo kumfurahisha mwafrika?kuhusu ushawishi wake, litakuwa swala la muda tu, kwani ameshawahimiza wapigane jihadi mpaka sasa hawajaanza kutekeleza zaidi ya yeye kupigwa risasi.(kwa wale wanaoelewa nini maana ya jihadi). . ukweli utabaki pale kuwa matendo ya mtu ndio imani yake.pia ni vigumu kumtenganisha mtu, anapokuwa maarufu kupitia ama kutokana na kuzuka kwa migogoro fulani na tabia yake au mwenendo wake. huyu jamaa anawahamasisha wapigane jihadi dhidi ya askari akidai wasiwaogope wao na virungu vyao kwani ni watu kama wao, wakati anajua askari wanamiliki sio virungu tu bali na bunduki na mabomu na pia polisi wenye imani yake na pengine wanaopenda na kuvutiwa na mihadhara yake pia wapo na aijipii mwema ni ndugu yao kama ilivyo ada. ugomvi hapa ni maslahi tu na sio mungu, inahitaji hekima kugundua hili na sio elimu pekeee manake hata uelimike vipi si rahisi kubadili mapenzi ya kitu.anachofanya huyu ni kuwapa watu kitu roho inapenda kusikia. na kuwapa excuses za maisha yao, kwamba bila fulani na fulani wasingekuwa hapo walipo nakadhalika nakadhalika. lakini ni swala la muda tu. kwakuwa ukweli siku zote ni mtakatifu, utaendelea kusimama. nisije sema sana mpaka huu uzi ukamwagiwa tindikali. lakini, naheshimu maoni yenu pia. Jk aliwahi kuwaambia ukweli, pale dodoma, wakati fulani nashawishika kuhisi kuwa labda watoto huwa wanadeka kwa baba yao, manake baba yao pia mpooooooole
 
viongozi wa nchi hii hawana uzoefu wa kutatua changamoto za taifa hili na ndio maana nchi imeendelea kuwa reactive na sio proactive katika mambo mengi. mfano madawa ya kulevya, ajali barabarani, njaa, huduma za afya elimu mbovu, magonjwa n.k.
kuna msemo unasema ukitaka kujua tabia ya mtu ni pale anapokutwa na tatizo. nchi zetu za kiafrika zinatatizo la kimfumo, . kipindi beni anaiacha nchi inapesa lakini haijatikiswa na changamoto mpya na ndio maana mfumo wa askari wetu na wanasiasa kutekeleza sera zao za kibabe uko vilevile.mabomu hayakuanza leo kilichojitokeza ni kuripoti matukio kumeongezeka na hii ikawa changamoto kwao. tindikali haikuanza leo lakini sasa imefika hadi ulaya, nadhani tutatunga sheria na kuweka mkakati mzito sasa ili wazungu watuone tupo siriaz
 
Back
Top Bottom