Nani yupo sahihi?

ICUB4

Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
16
Reaction score
2
kati ya anayesema 'nyimbo' yangu nzuri na ' wimbo' wangu mzuri nani yuko sahihi na kwa nini?
 
Kiswahili ni lugha ya taifa,ngoja nisubiri wenye taifa lao waje kutusaidia.
 
Nyimbo - Uwingi (Utasema Nyimbo zangu nzuri)
Wimbo - Umoja (Wimbo wangu mzuri)
 
kati ya anayesema 'nyimbo' yangu nzuri na ' wimbo' wangu mzuri nani yuko sahihi na kwa nini?

Hizi tungo nazipangua kama ifuatavyo:

1. Nyimbo yangu nzuri

Nyimbo=jina katika Wingi

ya
ngu= Kivumishi kimilikishi
ya=Kiambishi cha awali cha idadi(moja)

nzuri= Kivumishi cha sifa na idadi(zaidi ya moja)

Kwahiyo katika upatanisho wa kisarufi tungo hii haileti mlinganyo ulio sawa kwani inachanganya wingi na umoja na kuufanya uonekane ni umoja.
"Hivyo basi msemaji wa tungo hii hayuko sahihi "


2. "Wimbo wangu mzuri"

Wimbo=
Jina katika Umoja

Wangu= Kivumishi kimilikishi cha idadi(moja)

mzuri= Kivumishi cha sifa na idadi(moja)

Tungo hii " Wimbo wangu mzuri" ina mlinganyo wa maneno ulio sawa kwani haichanganyi umoja na wingi na kuuita umoja pia utananisho wa kisarufi unapatana sawasawa.

Kwa hiyo msemaji wa tungo hii yuko sahihi


Bilashaka nimejitahidi kupambanua kwa undani kidogo.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…