AVRAM
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 616
- 885
Bondia kutoka Tanzania Hassan Mwakinyo ametangaza nia ya kutaka kupambana na bondia maarufu kutoka Uingereza Kell Brook.
Mwakinyo mwenye umri wa miaka 23 ambae aliushangaza ulimwengu wa masumbwi kwa kumtandika Mwingereza Sam Eggington mwenye miaka 24 katika raundi ya pili.
Pambano la Mwakinyo na Eggington la uzito wa kati lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano kubwa la Amir Khan dhidi ya Samuel Vargas. Khan alishinda kwa tofauti ya alama dhidi ya Vargas.
Mwakinyo aliweka rekodi ya kumtandika Eggington ngumi 96, ambazo 51 kati ya hizo alimchapa raundi ya pili ya pambano hilo, ambapo lilikuwa lina jumla ya raundi 10.
Katika ngumi zote alizomtandika Eggington, bado mzungu huyu alikua imara na hajawa na hata dalili za kuanguka chini, hivi hii maana yake ni nini, kuwa Hassan bado ana ngumi nyepesi nyepesi zidi ya wapinzani wake au Eggington alikuwa imara zaidi na mchezo ulimshinda kwasababu ya mbinu alizotumia Mwakinyo kumsambaratisha.
Mwakinyo aliingia katika uga wa Arena Birmingham, jijini Birmingham Uingereza kama mbadala wa bondia mengine aliyetakiwa kupambana na Eggington kushindwa kufikia vigezo.
Wachambuzi wengi wa masuala ya masumbwi waliliona pambano hilo kuwa rahisi kwa Eggignton ambaye alikuwa na rekodi bora zaidi.
Wakati Mwakinyo akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 11 na kupigwa mawili, mpinzania wake alikuwa ameshinda mapambano 24 na kupigwa manne. Eggignton pia ni bingwa wa zamani wa Uingereza, Ulaya na nchi za Jumuiya ya Madola.
Haikuchukua muda mrefu toka pambano lianze kwa Mwakinyo kufurumusha mvua ya makonde kwa Eggington. Mwakinyo alianza raundi ya pili kwa kasi aliyomaliza nayo raundi ya kwanza na baada ya kumsukumia makonde kadhaa bila majibu, mwamuzi wa mchezo huo Kevin Parker alilazimika kumnusuru Eggington kwa kumaliza pambano hilo.
Mara baada ya ushindi huo, Mwakinyo alisikika akiimba kuwa anata kupambana na bondia mwengine kutoka Uingereza, Kell Brook.
"Yeye (Eggington) aliingia ulingoni akiwa mwenye kujiamini sana. Nilitaka kuonesha uwezo wangu, sie wengine ni mabingwa pia lakini hatuonekani kutokana na mzingira tunayoishi," alisema Mwakinyo baada ya pambano hilo na kuongeza: "Nimefurahi sana kwa ushindi huu na nimeionesha dunia uwezo wangu halisi."
"Sasa nataka kupambana na Kell Brook, na nikishamchapa namtaka Amir Khan." Alipoulizwa kama wataweza kustahmili nguvu za Brook akajibu kwa kujiamini: "Kwani wanionaje?"