Pole, nakushauri kaa na watu wazima ambao wazazi wako wanawaheshimu washirikishe kwa hili kisha mkae pamoja na wazazi wakujulishe wanayoyajua kuhusu waliyokwambia, kuna vitu nyuma ya hayo maneno. Ila kwa tahmini yangu , hao wazazi wako ni 'wabaguzi' na wakitoka kuchagua makabila, watakuja dini, kisha uchumi, kisha elimu...mwisho wa siku utajikuta unaishi kwa kuwafurahisha wao... mwamuzi na mshauri wa ndoa ni MUNGU peke yake, ndo maana imeandikwa kuwa mtu ataachana na wazazi wake na kuungana na mke/ mume wake. Kila kabila lina mapungufu yake na faida zake, wewe unamuoa mtu na si kabila... "sifahamu njia kamili ya kufanikiwa kimaisha hasa, ILA nafahamu njia ya kutaka kufeli kimaisha ni kutaka kumfurahisha kila mtu"