Naogopa kuchunwa

mshahara wa polisi unaujua? endelea kumsaidia tu pengine akipata hiyo degree ataweza nae kuchangia siku moja
 
ningekuwa wewe ningetumia hata ID lakini unavyokuja live kabisa humu namna hiyo mshkaji anaweza kukatiza humu akakuta hii mada inadiskasiwa bila yeye kupewa malalamiko rasmi n that can be so damaging, imagine mimi nakufahamu long time since msalato na udsm, what about his friends wakiona wakamshtue? Halafu, life is all about kusaidiana hasa mnapokuwa mnataka kujenga future pamoja, yawezekana pia wewe ndo umejionyesha uko juu kwa kuwa una masters na kazi nzuri na gari, sasa mshkaji akaamua kujiachia. kama kweli unataka kuishi na huyo jamaa this is the time for you to set the standards and discuss together and agree. Haina haja ya kuvunja uhusiano kwa kuwa tu anatumia gari yako, you can sit down and discuss how to share the cost. All the best gal.
 
well said Gaga, yaani kuna watu wanapenda sana kujishebedua humu JF, yaani mi sionagi umuhimu wa mtu kuanza kusema mara mie nimesoma, mara nna gari mara nafanya kazi nzuri blah blah kibao. Mi nnachijua kua kama mtu anakuja kuomba ushauri hapa baada ya ushawishi wake kushindikana, yaani mtu unajifanya unampenda then unakuja kumwaga upupu hapa? hata siku moja hajawai kumwambia tabia hii inamkera then unkuja kuomba ushauri, yaani inakera some time bana.
 
unaogopa kuchunwa mbona kama unachunwa tayari?mueleze kwamba ungependa mshee cost za hio gari,kama anakupenda atakuelewa akiwa mkali ujue yupo kimaslahi zaidi kwako,kusuka ama kunyoa ni uamuzi wako...
 
Dada Carmel umenena vyema hana lolote huyu zaidi ya kuja ku show off tu hapa.
 

Nafahamu long tm km hyo sio ID kwani kuomba ushauri vibaya, we toa maon pita wache na wenzio watoe yao.
 

Kutokana na uzoefu wangu - japo kwa kuona yanayowatokea watu ninaowafahamu - huo uhusiano hauwezi kudumu hata kama unautaka unless unaweza kumvumilia (kitu ambacho sikioni maana tayari umeanza kukerwa - na kumbuka mkiji-commit zaidi mambo mengine ambayo hujaanza kuyaona sasa hivi yatajitokeza). Jiulize, unaweza kuishi na huyu mtu akiwa na tabia hizo alizo nazo na juu ya hizo - ambazo huzipendi? Kumbuka watu wengi huwa hatubadiliki, naweza kujitahidi ku-accommodate unavyovitaka mwanzoni lakini si baada ya kukuzoea. Hebu fikiria: Kama hapa mwanzoni ndiyo anafanya hivi, huko baadae itakuwaje? Halafu kumbuka, Polisi wetu hapa Bongo (of course si wote kabisa - ila walio wengi, at least ninaowafahamu mimi) wanaamini kupewa vitu vya bure, aliewahi kujikuta na polisi sehemu za ulevi ataungana nami katika hili.

Jambo la pili:

Mara nyingi ndoa/uhusiano unaohusisha mwanamke msomi/breadwinner na less educated man huwa mchungu sana. I would say such relations almost always never work out. Ninamfahamu bwana mmoja (ni darasa la nane) ambae huwa anampiga mke wake (ni graduate) ili tu kumuonyesha "Nani ni mwanaume ndani ya nyumba hii"!

Najua kuna uwezekano wa kupigwa mawe kwa hili nitakalolisema ila Ladies out there you have got to know this: Most ( I insist not all) of Tanzanian men who have not been fortunate enough to be educated suffer from an acute inferiority complex especially when faced with ladies who are rich and educated.
 

Asante kwa kuwa na ujasiri wa kuweka private life yako hapa kwa ushauri. Kwa sababu hapa JF tuko watu wa aina mbalimbali tegemea ushauri wa kila namna, ila ni juhudi yako kuchukua lililojema

Nitajitahidi ku-discuss sehemu nilizo-highlight kwa rangi

1. Hapo kwenye blue, ninaona wewe mwenyewe huridhiki kuwa na huyu POLISI kwa sababu tu una elimu kubwa

2. Hapo kwenye RED, hicho ndo kilichokufanya umkubali huyu jamaa.. huenda ulimlazimisha au alikuingia kwa gear hiyo..
Kumbuka kuna ku-DISCO

3. Hapo kwenye BOLDED BLACK, hapo ndo nimeona makucha yako, ni kwamba unapenda ushauriwe umuache au uendelee KUVUMILIA (nafikiri huijui vizuri definition ya kuvumila)

Hivyo basi ninashawishika kusema kwamba SIONI mapenzi ya kweli kutoka kwako kwenda kwa Polisi wako.
Na hii ni hatari huko mbele ya safari, kwani mtakuwa ni watu wa kulambana, maana kwa kisa kama hiki nilitegemea kwa msichana mwenye elimu kama wewe, ni kitu kidogo sana kama ungekuwa na upendo wa kweli kwake.

Inawezekana Polisi wako ni handsome, au unaogopa tu kwa sababu yeye ni polisi, na hivyo huenda hujapata mwanamume mwingine aliyeonesha interest ili um-bwage mtu wako.

Nakushauri usifanye mchezo wa kitoto.. JIULIZE kama ni kweli unampenda, na atafaa kuwa mume wako kulingana na vigezo vyako..
Kama hupati jibu ni bora ukamwambia atafute msichana mwingine.

Kwangu mie, kisa kama hiki kama kweli mnapendana ni jambo la kukaa chini na kujadili na kuwekeana mipaka..

All the best na pasaka njema
 
Dada huna mapenzi ya kweli kabisa, watu wanatoa Gari mtu anaenda kulala nalo itakuwa kuendesha tu? ukiwa na mapenzi ya kweli hiki kitu ni minor kabisa. jiulize deep inside unampenda au ndio umejishikiza? na kwa nini ujishikize hujiamini kama utapata unayempenda mnayeendana? Ndoa sio dili sana vumilia mpaka wakati wako ufike
 
mtu anaomba msaada wa mawazo wewe unasema ana-show off..wewe mbona hujaleta visa vyako..tujaribu kujadili kwa ustaarabu..leo kwake kesho kwako..
hebu nisome vizuri utanielewa sio unakurupukia mambo wewe
 

yaani gaga sijui nikupe nini jamani!
 

Dada inamaana we hujui police walivyo?wanajua kupokea tu hawajui kutoa,kwa hiyo swala la kupewa futa kabisa.
 

No hebu fanya kinyume chake ingekuwaje?
 
Dah!! Ngoja kwanza nimshukuru ma'wife 2 be kwa moyo wake wa chuma ,Ushauri wangu kwako ni huu Jiulize maswali matatu ya msingi_

KWANZA KABLA YA YOTE FUTA HII POST YAKO NA UENDELEE KUAMINI ULICHO AMINI MWANZO NA USIZIRUHUSU HISIA MFU.
Na ujiulize
Upo tayari kuingia kwenye mahusiano ya kudumu?
Ungependa kuanzisha mahusiano na mtu wa kiwango gani kiuchumi ,kelimu, kijamii?
Uulize moyowako kwa kumshirikisha Mungu kweli huyu nichaguo lako i mean anasifa unazo zihitaji ?
Kama jamaa akijizolea max za kutosha amini ndiye.

Nakushauri ujifunze kujitegemea kiakili yapo mambo ya kutaka ushauri lakini si ya kimaamuzi otherwise mi nauita ushamba tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…