Mechanic 97
JF-Expert Member
- Feb 6, 2021
- 854
- 1,296
Wakuu, ninakaribia kutimiza mwaka tangu nihamie sehemu hii ninayoishi sasa. Lakini hali niliyokutana nayo hapa inaniumiza sana, hasa kutokana na biashara ninayotaka kuanzisha. Biashara hii inahitaji niandae bidhaa, lakini sina ofisi na kwa mkoa huu ninapoishi, gharama za kuwa na ofisi ni kubwa sana, na sina uwezo kifedha kwa sasa.
Hali iliyopo ni kwamba naishi kwenye ghetto, lakini tatizo ni kwamba nilipofika hapa, nilianza kwa kufanya kazi yoyote iliyokuja bila kuchagua, hivyo watu wameshanizoea kwa mtazamo huo. Shida inatokea pale ninapokuwa geto, kwani kila mara nikiwa hapo, watu wananiuliza kama nipo tayari kwenda kufanya vibarua vya muda.
Hapa ndipo matatizo yangu yanapoanzia, kwa sababu ninapata changamoto ya kuepuka vibarua hivyo na kuzingatia biashara yangu, ambayo ninaona ina tija zaidi kwangu. Kwa sasa, nimekuwa nikifikiria kwenda kuangalia mazingira ya SIDO, lakini sielewi vizuri utaratibu wa kujiunga nao.
Naomba yeyote anayejua mwongozo wa kujiunga na SIDO au mbinu za kuepuka vibarua ili niweze kufanya shughuli zangu zenye manufaa zaidi anisaidie tafadhali.