tian Nakuelekeza tu bila vipimo. Vipimo hadi siku nikipika.
Changanya unga + chumvi + sukari kidogo km kijiko kimoja + iliki + samli iliyoyayushwa / mafuta+baking powder kidogo
Changanya vizuri fikicha usiwe na madonge Weka tui zuri au maziwa kwenye mchanganyiko taratibu huku unakanda hadi upate donge moja (lisiwe gumu na wala laini kupitiliza ) liweke pembeni km robo saa. Chukua unga ukate madonge halaf Tengeza minyororo mirefurefu ukate kwenye kibao ( ukipenda kutengeza shape tofaut unaweza kuchukua chujio au grater baada ya kukata uvigandamizie kidogo )
Teleka karai la mafuta uvichome hadi viwe golden brown. Viwache vipoe.
Tengeneza shira kutumia sukari + maji + iliki / vanilla Chemsha hadi iwive, ili kujua km imewiva vizuri ukiigusa utaina inanyamata au ina uzito flani hivi Au njia nyengine chukua kikomba weka maji kidogo halafu tonyeza ile shira ndani ya kikomba utakuta lile tone limeenda moja kwa moja kukaa chini ya kikombe.
mimina vile visheti vyako vilivyopoa huku ukivipetapeta.
Km shira iliiva vizuri utaona vimekauka mara moja .