Naomba kuelekezwa namna ya kuanzisha online TV

u

Hivi ile laki moja kama unaanza ni unalipia kwa mwaka mzima au hio ni kwaajili ya usajili tuu ile laki tano ipo pale pale
Laki moja ni kwaajili ya application tu yani ili waitazame channel yako,wakishaona inafaa kupewa leseni ndipo wanakupa control namba ya kulipia leseni ambayo ni laki tano.
 
Hujaongelea jinsi ya kupata revenue
Revenue ni swala pana sana but nitaeleza kwa ninavyoelewa

Njia kuu ya revenue kwa youtube ni Adsense,na inatakiwa upate subscriber 1000 na watch hour 4000 ndani ya miezi 12,ambavyo ndio vigezo vya wao kukupa matangazo au kwa lugha nyingine kukukubalia kupata huduma ya adsense.

Ukishapata sasa hela inatokana na yale matangazo ya kwenye video yako,mfano ukiona tangazo la cocacola,means coca wamelipa wla youtube,sasa ile hela wewe mwenye video unachukua 60% na youtube wanachukua 40%

Uwingi wa hela utategemea nchi unayotazamwa sana,mfano watazamaji wako wakiwa wengi kutoka tanzania,manake inatumia COST PER MILE (CPM) ya Tz ambayo hii CPM ni kiwango unachopata watazamaji 1000 wakiangalia video yako na kuona tangazo.

Sasa CPM ya bongo ni ndogo,huwa inacheza $ 1.2 kushuka chini,mqnake watu 1000 wakibongo wakiangalia video yako unaweza pata $1.2 au chini ya hapo.

CPM za nchi za kinagharibi ni kubwa,mfano marekani CPM yao huwa inafika mpaka $8 manake ukiwa na watazamaji 1000 wa marekani unapata dola 8 au zaidi ndio maana youtubers wa nje wana hela nzuri hata wakipata views kidogo.

Kila nchi ina CPM yake na pia CPM hubadilika badilika mkuu.

Naimani umenielewa kwa uchache.
 
Naomba utofauti wa YouTube partnership program na Google AdSense katika kuingiza pesa kupitia YouTube channel
 
mkuu kwa mawazo haya utagawa tigo unawaza vitu vikubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…