Naomba kuelekezwa, nataka kununua Kiwanja

Naomba kuelekezwa, nataka kununua Kiwanja

Ynamo

Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
21
Reaction score
6
Habari wanajukwaa.
Ninataka kununua kiwanja naomba kuelekezwa ni vitu gani vya msingi kisheria ambavo natakiwa kuvifanya.
 
Kina hati???

Kama kina hati anzia kupiga search ardhi

Kama hivu vya holela shirikisha serikali ya mtaa....majirani nk maana serikali ya mtaa wenyewe hawaaminiki sana siku hizi
 
Kama unataka kununua kiwanja jiridhishe yafuatayo:
1. Kinamilikiwa na watu wengi au mmoja (Epuka kuziwa mali ya mali ya watu wengi bila ya kuwashirikisha wahusika wote)
2. Hakikisha hakina mgogoro kwa kuuliza majirani au wauzaji au ungozi wa mtaa husika.
3. Kama kina hati unashuriwa ukafane title search kwa msajili wa hati.
4.Hakikisha unafanya malipo yote pale title deed transfer inapokubaliwa na kamishna wa Ardhi. Usili pesa yote mpaka transfer ipite kwani inawezekana nyaraka ukapewa feki.
 
Kununua kiwanja ni process ndugu...
1. Ufanye verification kama hicho kiwanja kipo ama la....
2. Baada ya kujua kama kipo then inapaswa ufuatilie kwa undani kwa kumuhoji huyo mmiliki. mfano, kina hati? yeye alipaswa kumiliki kwa miaka mingapi na mingapi imebaki? Ni cha urithi ama? kwanini anauza nk nk...
3. Baada ya hapo inabidi upige official search ambapo utaomba kwa kamishna wa ardhi. Yeye atakupa jina sahihi la mmiliki na muda wa umiliki nk...
4. Utanunua ardhi yako...
 
Back
Top Bottom