Naomba kueleweshwa Kuhusu Dyslexia, hivi huu ni ugonjwa, hali au ni nini?

Naomba kueleweshwa Kuhusu Dyslexia, hivi huu ni ugonjwa, hali au ni nini?

Jorge WIP

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2018
Posts
3,567
Reaction score
5,323
Maana yake
“Dyslexia is a learning disorder that affects a person's ability to read, write, spell, and speak.
It is a neurological condition that makes it difficult for people with dyslexia to process language in a typical way.
Dyslexia can affect people of any age, race, or gender, and it is estimated that up to 15% of the population has some degree of dyslexia”

Nna kijana hapa anapata taabu kwenye kuelewa ukimfundisha anakuwa mgumu kuelewa ni mwanafunzi wa secondary ila anaandika kama mtoto wa Primary Mfano neno “saw” yeye ataandika “was”

Naomba msaada kwa wataalamu nifanye nini ili kijana aweze kuandika na kusoma vizuri zaidi.

Sina uhakika kama ni Dyslexia maana mimi sio daktari ila hizo dalili zilizotajwa hapo naona zote anazo.

Ahsante
 
Jorge WIP niliwahi kuandika jambo kuhusu ugonjwa huu. Hivyo nitakopi na kuoost hapa kila kitu.

___

Kutokana na uelewa na muamko hafifu wa elimu ya malezi ya watoto from prenatal to postnatal (Psychology) kuna mambo hua yanawakumba watoto na wazazi bila kuelewa wanachukulia ni swala la kawaida mtoto kua hivo. Wengine wanaweza ihusisha hali Fulani aliyonayo mtoto na maswala ya nguvu za giza kumbe sio kweli, ni mtoto anakua anahitaji uangalizi na huduma ya kiasaikolojia ili kuondoa hali yoyote isiyo ya kawaida aliyonayo mtoto.

There’s this person I know mtu mzima tu ukiongea nae ana tatizo la kusahau maneno, kuna yale maneno common tunayotumia siku zote kwenye maongezi yeye inakua shida kwake kuyajua mpaka anaulizia labda kufanya kitu falani wanaitaje? Unaweza kujua anajifanyisha au ndio mapozi yake ya mazungumzo but ndio yuko hivyo hua hajui maneno so ukizungumza nae inatakiwa umchukulie kama alivyo…Yeye binafsi anaona ni jambo la kawaida kwamba ndio alivyo lakini in reality ana tatizo ambalo kwa umri aliofikia natumaini haliponi tena.

Nikiwa shule ya msingi japo sikufanikiwa kusoma chekechea na niliomea shule za st kayumba toka kwa walimu wa UPE ila ndani ya miezi 6 ya kwanza nilikua nishajua kusoma vizuri tu na nalikua nawaelekeza wenzangu jinsi yakusoma na kuunga maneno. Niliwahi zaidi na mpaka leo nina speed kubwa sana kwenye kusoma vitu, shida yangu ilikua kwenye kuandika tu. Nilichelewa kujua kuandika maneno kwa ufasaha na nina muandiko mbayaaaa sana bora sasa kidogo umebadirika, nilikua naandika minyoo minyoo mwandiko wangu nadhani ni mimi na mwalimu ndio tuliweza kuusoma ……nimeweza kujua kuandika vizuri nikiwa darasa la 4 baada ya kupigwa sana sana na mwalimu wa Kiswahili hopefully mwafahamu jinsi walimu wa 90s walivyokua wanatandika bakora. Mpaka leo hii naandika hapa namba 2,3,8,5 na herufi g, y,r k siwezi kuzinadika vyema. Lakini kwanini mtu huyo ashindwe kufahamu maneno ya kawaida tu yanayotumika kila sikua na mimi kwanini nishindwe kuandika vyema?

Dyslexia ni tatizo ambapo muhusika mwenye tatizo hili anakua inamuwea vigumu kuandika na kusoma ajili kushindwa kutambua sauti za matamshi, Wernickes’s area ni sehemu inayopaktikana kwenye posterior superior temporal lobe ambayo ipo kwenye ubongo wa mbele. Katika eneo hilo ndio kunahusika na kuchakata matamshi kama yameandikwa au yametamkwa, hivyo basi Dyslexia hushambulia eneo hili linalohuika na kuchakata lugha.

Kwakawaida dalili za huu ugonjwa hua ni ngumu kuugundua kabla ya mtoto kuanza shule lakini kuna baadhi ya viashiria ukiviona kwa mtoto basi vitakuashiria kwamba mwanao pindi akifianza shule anaweza kua na tatizo hili. Zifuatazo ni dalili za ugonjwa huu

Kabla ya kuanza shule
Hivi ni viashiaria amabavyo mwanao anaweza kuvionyesha kabla ya kuanza shule ambavyo vitakuashiria kwamba mwanao akianza shule atakua na dyslexia.
Kuchelewa kuanza kuongea
Kujifunza maneno mapya taratibu
Kushindwa kukumbuka kwamba hii ni namba ngapi au herufi gani, kushindwa kutambua rangi
Kushindwa kuunda maneno kwa usahihi pindi anapotamka au kuchanganya maneno ambayo yanafanana katika matamshi

Akianza shule
Hizi ni dalili ambazo mwanao atazionyesha pindi atakapoanza shule
Kushindwa kutambua na kuelewa kile anachosikia
Kusoma chini ya kiwango alichotarajiwa
Kushindwa kutambua neno sahihi au kuunda jibu la kitu anachotaka kujibu/kutamka
Kushindwa kukumbuka mfuatano wa vitu. Mfano mtoto anashindwa kukukumbuka kua baada ya 5 inafuata 6 au baada P inafuata Q
Kushindwa kuona au kusikia ufanano na utofauti uliopo kati ya maneno na herufi (kama neno “mama” yeye atalitaja herufi moja moja na kama ni herufi "m" yeye atalitaja mama)
Kuchukua muda mrefu kumaliza kazi ambayo inahusiana na kuandika au kusoma
Kushindwa kutaja spelling /herufi za maneno
Kukwepa kufanya kazi zinazohusiana na usomaji

Kwa vijana na watu wazima.
Kijana au mtu mzima mwenye ugonjwa huu hua na sifa zifuatazo au huonyesha dalili zifuatazo
Kushindwa kusoma vzuri hasa kwa sauti
Kusoma au kundika taratibu
Kushindwa kutaja herufi za maneno/spelling
Kukwepa kufanya kazi zinazohusiana na usomaji
Kutamka maneno vibaya au kushindwa kutoa maneno pindi anapoongea
Kushindwa kuelewa matani, au kuelewa maneno ambayo maana yake imefichwa hasa nahau.
Kutumia muda mrefu kusoma au kundika
Hua hawawezi kufupisha story pindi anapohadithia jambo
Inakua ngumu kwao kujifunza lugha mpya
Kushindwa kukumbuka yale waliyoyasoma
Kushindwa ku-Solve maswali ya mafumbo kwenye hisabati

Hivi maana halisi ya neno Disorder ni ugonjwa au tatizo? Maana mara nyingi kitu kikiitwa Disorder hua hakina tiba ya dawa , mara nyingi hutibiwa kwa kuonana na wataalam wa saikolojia. Hili tatizo la Dyslexia hua hauna tiba. Kwa wenzetu wanakua na program maalumu ya kuwaelekeza vyema kutokana na hali yao na huku kwetu hua kuna program yao maalum ya kutandika bakora wanafunzi wasioweza kusoma vyema na kuandika mnyoo/wakama bata kapita kwenye daftar kama mimi.

Kumchapa mtoto kwamba haujui kuandika vyema bila kujua cahnzo cha yeye kuandika hivyo kunamfanya mtoto azidishe hofu ..hofu inampelekea ashindwe zaidi. Acheni kuwazonga watoto zenu kua wana”hati” mbaya bila kujua sababu husika, kaeni nna watoto zenu muwachunguze matatizo waliyonayo bila kuwafokea na kuwachapa. Hili tatizo hua linarithishwa au anaweza kulipata pindi akipata ajali ya kichwa. Ukosefu wa eleimu ya saikolojia kwa wazazi wetu umetufanya sisi watoto zao tunaoelekea kua wazazi kuishi kwa shida kiakili kutokana na Trauma tulizopata kutoka kwa wazazi na walimu. Natumaini watoto zetu watalea vizuri watoto wao kadri ya misingi ya malezi kisaikolojia inavyoagiza ili kuepusah trauma kwa watoto zao kama tulivyozipata sisi wazazi.

Je kuna yeyote aliyegundua kama ana tatizo hili au mwanae?? Shea nasi jinsi unavyokua tujifunze. We scare because we care

-Vinjii
 
Maana yake
“Dyslexia is a learning disorder that affects a person's ability to read, write, spell, and speak.
It is a neurological condition that makes it difficult for people with dyslexia to process language in a typical way.
Dyslexia can affect people of any age, race, or gender, and it is estimated that up to 15% of the population has some degree of dyslexia”

Nna kijana hapa anapata taabu kwenye kuelewa ukimfundisha anakuwa mgumu kuelewa ni mwanafunzi wa secondary ila anaandika kama mtoto wa Primary Mfano neno “saw” yeye ataandika “was”

Naomba msaada kwa wataalamu nifanye nini ili kijana aweze kuandika na kusoma vizuri zaidi.

Sina uhakika kama ni Dyslexia maana mimi sio daktari ila hizo dalili zilizotajwa hapo naona zote anazo.

Ahsante
Kama ni Dyslexia kweli basi haina tiba, anahitaji uangalizi wa karibu na kumuelekeza bila kuchoka
 
Ilishakua tatizo tangu azaliwe.. Inaeza kuendelea kudevelop kwa namna tofaut anavokua..
Ni kama watoto wenye cp..
Ni kupambana nae tuu bila kuchoka kwa kuwa umeshaijua hali yake.. 👏
 
Kama ni Dyslexia kweli basi haina tiba, anahitaji uangalizi wa karibu na kumuelekeza bila kuchoka

Najitahidi lakini sasa shida nna hasira kidogo, Mungu atasaidia itabidi nitumie new approach
 
Ilishakua tatizo tangu azaliwe.. Inaeza kuendelea kudevelop kwa namna tofaut anavokua..
Ni kama watoto wenye cp..
Ni kupambana nae tuu bila kuchoka kwa kuwa umeshaijua hali yake.. [emoji122]

Sawa ndg yangu.
 
Najitahidi lakini sasa shida nna hasira kidogo, Mungu atasaidia itabidi nitumie new approach
Aisee mkuu nenda naye taratibu, jaribu hata kusoma vitabu mbali mbali kujua namna ya kumuwezesha, mara nyingi hao madogo huwa na kitu cha ziada ila kutokana na jamii kutofahamu jinsi ya kuwafundisha huwa wanawekwa kwenye kundi la wanaofeli darasani

images (92).jpeg
 
View attachment 2539805

Ntajaribu kulifuatilia kwa kina hili. Thanks to LinkedIn nilikutana na post ndio nkaunganisha dots
 
Hii Umeitendea haki maeleozo mazuri sana ya kumfanya mtu apate pa kuanzia, wazazi na walimu wengi hawako aware na Dyslexia na hii Inapelekea watoto wengi kumaliza shule hawajui kusoma na kuandika
 
Back
Top Bottom