Naomba kueleweshwa kuhusu fedha zinazotumika kujenga mradi wa SGR

uncle

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2007
Posts
325
Reaction score
184
Kuna suala naona silielewi kwenye ujenzi wa SGR kila Rais Magufuli anapohutubia hupenda kujipambanua kuwa mradi wa SGR serikali inatumia fedha zake za ndani.

Lakini kwa kusoma sehemu mbalimbali naona kama tunakopa hela toka Mabenki ya nje mfano kipande cha Dar - Moro, kuna hela zimetoka mabenki ya Uturuki na Leo hii nimesoma kuwa Standard Chartered Bank wametoa hela kwa ajili ya kipande cha Moro- Makutupora.

Sasa huo mchanganyiko siuelewagi kabisa
 
Kaka ikifika kipindi cha kulipa deni tunalipa wote kwa kufunga mikanda
@uncle madeni yapogo tu miaka yote usihofu. kwa rasilimali zilizopo Tanzania na usimamizi wa mapato ukiwa mzuri madeni yatalipwa na nchi itasonga kwa kasi yamwanga.
 
Ni simple tu; kwani anaposema corona imekwisha unafikiri ni kweli hakuna corona au ni propaganda za kisiasa tu? Kwa yeye kuwa rais huwa anafikiri watanzania wote ni wajinga sana.

Hata mawaziri wake kila siku wanadhalilika kwa namna anavyowatendea, ni propaganda tu hakuna wakati nchi imekuwa na madeni makubwa kama awamu hii.
 
Wewe ukikopa hela inakuwa siyo ya kwako sio? Au ukikopa huwaga Hulipi? Tofautisha Grant na Loan hiyo Mikopo Tutailipa sisi sisi wananchi hivo tunajenga kwa Pesa zetu ni kama wewe leo ukope Bank afu ujenge nyumba utasema bank imekujengea nyumba au utasema nimejenga nyumba?
 
Semeni ukweki kwamba tunajenga kwa fedha ya mkopo idiot
 
Jiwe,Kabudi na Pole Pole wanasema SGR inajengwa kwa hela za ndani tena cash money,tena Jiwe akaenda mbali zaidi kuwakashifu watangulizi wake hasa Kikwete kwa kukopa hela na kufanya miradi ya maendeleo.
 
Hii nchi ngumu hakuna utakachofanya ukakubalike.

Hela ingeweza kutoka na kazi isifanyike, sijui hapo tungesemaje.

Hongera sana Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli,

Fanya kazi tu, pengine thawabu utapata Mbinguni siyo duniani hapa.
 
Jibu hili hapa leo;

 
Magufuli anajuwa kuwa anatawala Watanzania ambao ndiyo watu wenye uelewa mdogo kuliko wote katika Afrika Mashariki. Ndiyo maana anakopa Benki za nje mnashanglia. Na siku ya uzinduzi anasema tumejenga kwa hela zetu mnamshangilia pia
 
Safi sana mkuu
 
 
Hii nchi ngumu hakuna utakachofanya ukakubalike.

Hela ingeweza kutoka na kazi isifanyike, sijui hapo tungesemaje.

Hongera sana Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli,

Fanya kazi tu, pengine thawabu utapata Mbinguni siyo duniani hapa.
Umeielewa mada kweli?
 
Na huo ndio ukweli wenyewe....
Au nasema uwongo ndugu zangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…