Naomba kuelimishwa jambo hili kuhusu afya ya figo

Naomba kuelimishwa jambo hili kuhusu afya ya figo

chinatown

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
1,232
Reaction score
1,105
Nafahamu utendaji wa figo, kuchuja uchafu na vitu vinginge vilivyo katika damu na kutoka kwenye mwili wa binadamu kwa njia ya mkojo.

Na hii hufanyika mara thelathini na ushee hivi kwa masaa 24, nataka kujua hiki ambacho nime experience kwangu, mara zote nikiamka asubuhi na kwenda kupuu mkojo huwa colored kama chai ya rangi au inayoelekea huko, lakini nikioga tu mara nyingi sio zote huwa nasikia mkojo ambao huwa kidogo >200mls unakuwa clear kabisaa.

Nataka kujua mechanism ya figo hapa maana nilitegemea kuendelea kupata mkojo colored maana ninakuwa bado sijanywa kimiminika chochote muda huo, nilitegemea labda baada ya kula au kunywa ndio nipate clear urine.

Michango yenu tafadhari!
 
Rangi ya mkojo inabadilika kuanzia chini kwenda juu,iko hivi,mkojo unaokuwa umetangulia kwenye njia ya mkojo kabla ya kutoka ndio unakuwa na rangi ya njano sana/hiyo yarangi ya chai,lakini kadiri unavyopanda kwenda ndani unakuwa mweupe zaidi,kwahiyo ukishatoka ule wenye rangi unaofuata ni ule mweupe ila hapa kuna factors,kama hunywi maji mengi rangi itaendelea kuwepo,ila kama unakunywa maji ya kutosha ni ule wa kwanza tu ndio utakuwa na rangi unaofuata utakuwa mweupe,na hii hali ya utofauti wa rangi mara nyingi unaweza kuiona ukiwa umebana mkojo kwa muda mrefu...
 
Back
Top Bottom