[QUO
Tofali hutofautishwa kwa njia zifuatazo
1.Aina ya material yaliyotumika kuiunda mfano kuna tofali zinatengenezwa kwa
Maji, Simenti na Mchanga
Maji, Sementi na Vumbi la miamba uiliyosagwa kwa wakati wa kuzalisha kokoto
Maji, Sementi na Chenga za kokoto.
Maji na Udongo Mfinyanzi baadae inachomwa hapa unapata tofali za kuchoma.
Kiujumla material yapo mengi na wanasayansi/watafiti kila Leo wanaendelea kutafiti material mengine kulingana na teknolojia inavyobadilika na kukua.
2. Njia nyingine ya kutofautisha ni compression strength ambayo mara nyingi inaanzia 0Mpa mpaka 14Mpa hii hufanyika maabara unafyatua tofali kwa material niliyojaribu kuelezea hapo juu.
Mfano kwa mfuko mmoja wa Sementi umetoa blocks 25 mwingine akaamua kutoa blocks 40 ukipima hizi tofali zitatofautiana strength.