Naomba kuelimishwa kuhusu sheria za minada

wakurochi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
2,647
Reaction score
2,951
Hapa mtaani kwetu sasa hivi mnada umeahirishwa. Ilikuwa ipigwe mnada nyumba ambayo wenye nyumba walikopa 10m na dhamana ikawa nyumba. Nyumba yenyewe kwa tathimini ya muonekano inazidi milioni 80.. Watu wamekusanyika baada ya matangazo kama kawaida. wakati watu wanasubiri mnada, mtangazaji wa mnada akaingia ndani ya nyumba iko ndani ya ukuta na geti kubwa. Akatoka baada ya mazungumzo humo ndani na kutoa taarifa watu watawanyike mnada umeahirishwa wadaiwa wameomba wapewe muda zaidi watsmaliza deni.
Naomba kujua kama hii imekaa sawa ,kwasababu siamini Lugumi kama angeweza kuahiridha au kuna mazingira yanayoruhusu.

Nawasilisha
 
Dalali + Bank + Mdaiwa wana uwezo wa kuahirisha zoezi tajwa mara tuu wakisharidhiana juu ya ulipwaji wa nkopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…