Naomba kuelimishwa ni kwanini Makamu wa Rais Samia hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli?

Lucas Mimi Si chawa mwenzio,

Nimekushauri pima ulichokiandika kabla ya kupeleka public,

HOJA Yako unalazimisha watu waulize maswali ambayo majibu yake kamwe hayawezi kupatikana Kwa sababu maalum.

Pima uzito wa kinywa chako kabla hujaongea Lucas.
Huyu chawa upeo wake ni mdogo sana yeye anachofikiria ni uteuzi tu.
 
Rais Samia Ni Akili kubwa,ni kiongozi mwenye maono,upeo na uzalendo wa hali ya juu sana. Ni kiongozi mchapa kazi sana na ndio maana hata jenerali Venance Mabeyo amempongeza kwa ulimi wake mwenyewe.
Hujajibu hilo swali langu la msingi, fanyia kazi homework hiyo.
 
Pia inaonesha cheo Cha Makamu wa Rais ni cheo Cha maigizo kisicho na maana.

Yaani Waziri Mkuu ndio anapata nafasi ya kwanza kabla ya VP? Haikubaliki kina haja ya kubadili sheria au kufuta hiki cheo
Nafasi ya MwR kipo kisiasa tu, tena kwa sababu ya muungano ili kubalance equation ya muungano ila hakina maslahi yoyote kwa taifa. Ni hasara kw ataifa kuwa na MwR na WM kwa wakati mmoja, huyo mmoja yupo yupo tu.
 
Makamu wa Rais wetu ni cheo cha kisiasa, ila hakina mamlaka. Ndiyo maana hawatengui uteuzi na wala hawateui.

Pia, ieleweke kubwa Rais anapokuwa mgonjwa, ndipo ratiba ya kazi ya Makamu wa Rais huongezeka zaidi ya awali, za kwake na za Rais.

Majukumu ya nchi lazima yaendelee, maana maelezo yako yamekuwa kama unadhani Makamu wa Rais ni mke wa Rais.

Kwamba Makamu wa Rais awe kando ya kitanda cha hospitali cha Rais na afute ratiba zote za kazi. Hili nadhani si sawa. Kazi lazima iendelee.

Ova
 
Unaachaje bosi wako kitandani anapigania uhai wake wewe unakwenda kupiga posho za ziara Tanga? Waliotaka asiapishwe Wana hoja.
 
Nafikiri hapa ni vitu viwili tofauti. Kama rais wa nchi Janeth hahusiki na taarifa. Ila kama Magufuli angekuwa mume wa Janeth tu bila kuwa Rais taarifa ya kwanza ingemhusu. Ila pale Magufuli alikuwa anauguzwa na nchi, siyo mambo ya kifamilia yale

Kahiyo Magufuli alivyokuwa anaumwa taarifa ya kwanza ilipewa nchi? Kumbuka Katelephone alisema Rais yupo fiti anachapa kazi ,katika kipindi cha rais anachapa kazi(kwa mujibu wa katelephone) ina maana Janeth alikuwa hajui kama yupo Mzena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…