Naomba kuelimishwa ni kwanini Makamu wa Rais Samia hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli?

Afadhali wewe umejibu hoja na siyo yule ccm Rabbon ndugu yake Lukas alikuwa anamtisha.

Hapa Lukas ndo ajue na aelewe kuwa wanaposema kuwa ccm wengi wanajivika uchawa wakidhani kuwa ndo kufia chama kumbe wasijue kuwa wanabomoa. Hapa amepata elimu kwa asiye chawa na s kama alivyokuwa anatishwa na Rabbon.
 
Hata mimi ningekuwa Samia ningeshughulika sana na wote waliotaka kupindua katiba..... kwa maelezo ya CDF ni kuwa kwanza walitaka kubishia mwongozo wa katiba na baadae wakataka Rais aapishwe baada ya mazishi na mwisho kabisa wakataka kumuapisha kihuni bila utaratibu. Mimi ningewanyoosha na wangejuta maisha yao yote. Tunaposema Mama Samia ni mtu mwema asiye na visasi watu wawe wanaelewa.
 
Unaachaje bosi wako kitandani anapigania uhai wake wewe unakwenda kupiga posho za ziara Tanga? Waliotaka asiapishwe Wana hoja.
Sasa angefanyaje kama alikuwa amefichwa kupewa taarifa? Hujaona katika andiko langu nimeuliza kwanini walimpangia ziara Mh makamu wa Rais kwenda Tanga?
 
Watu wengine wajinga tu .eti badala akuelimishe anaanza kukupa vitisho utafikiri nchi hii ni ya wazazi wake.
 
Kwa sababu katiba haifatwi.

Na hata Samia huyu huyu haiheshimu katiba ndio maana aliita"KIJITABU"

Tunahitaji katiba itakayombana yeyote yule awaye madarakani akikiuka sheria na taratibu .

Katiba hii chakavu ya sasa ina miaka 47 imeshakuwa kama "past papers " za mitihani iliyowahi kufanyika hivyo even nobody no longer give a damn about it.
 
Unatumia kipimo gani ewe mnyamwezi na sisi tukakinunue? Kipindi Magufuli yupo walikuwepo Kama wewe walimwita the worst president..Mara dikteta uchwara nk. KWA HIYO HATA WEWE KUMUITA HATOSHI WALA SI AJABU NA WALA HUTAENDA KUKIKALIA KILE KITI kwa ufupi vumilia tu mpaka amalize wewe endelea kulima huko ushetu😃
 
Hoja yako ni ipi "wa kwanza kupewa taarifa" au "anayetangaza?"
Kuna mahala Katiba imeelekeza juu ya kupewa taarifa? Mkewe angekua wa kwanza pia kupewa taarifa ungelelalamika?
 
Hoja yako ni ipi "wa kwanza kupewa taarifa" au "anayetangaza?"
Kuna mahala Katiba imeelekeza juu ya kupewa taarifa? Mkewe angekua wa kwanza pia kupewa taarifa ungelelalamika?

..kwa hali aliyokuwa nayo Magufuli, Mama Samia alipaswa kuwa ACTING PRESIDENT.

..Na wakati wote Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Madaktari walipaswa kuwa wanampa Mama Samia taarifa za hali ya mgonjwa ili afanye maamuzi.

..hivi kwa mfano nchi ingevamiwa wakati ule, ina maana Kassimu, Venance, na Bashiru, wangeendelea na danadana zao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…