Naomba kufahamishwa fundi mzuri kwa jiji la Mbeya, Gari yangu ina tatizo la kugonga ninapofunga breki

Naomba kufahamishwa fundi mzuri kwa jiji la Mbeya, Gari yangu ina tatizo la kugonga ninapofunga breki

mwambyetete

Senior Member
Joined
May 17, 2018
Posts
132
Reaction score
202
Habari wapendwa, naomba msaada wa kupata fundi mzuri au ushauri juu ya tatizo linalonikabili kwenye gari.

Natumia gari aina ya toyota premio engine 1NZ,gari yangu ina tatizo la kugonga hasa ninapofunga breki yaani ninapokaribia kusimama kabisa au ninapoiondoa iwapo ilisimama kabisa!! Mlio ninaousikia huwa kama kakakakakaka naomba mnielewe hivo.

Nilipeleka kwa mafundi hawa wa mtaani wakadai plate za kwenye shockup zinazokaa juu ya coil zimelika na kufa hivo nibadilishe, tatizo halijapona.

Jana nikaambiwa top mount za kwenye shockup na balljoint zimekufa zimenunua zingine bado tatizo liko pale pale!! Tena nikaambiwa breakpad au steringleak imekufa sasa napata wakati mgumu kununua vitu hivo kwan n kama napiga ramli sasa.

Umri wa gari ni ya mwaka 2005 na had sasa imetembea km 80,000. Naomba mnisaidie au ushaur au wap ntapata fundi mzur wa kunitatulia tatizo hilo ambapo gari ni premio new model ya 2005 package F ya cc 1496.

Kimakazi niko mkoani Mbeya wilaya ya mbeya mjini!

Heri ya pasaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watafute Evolution Garage wapo maeneo kati ya Ilomba na Sae hiyo njia ya kwenda Uyole upande wa kulia unapokuja Dar.
Hiyo ni gereji ya kisasa na wana vifaa na mafundi wazuri.

Kwa mawasiliano wacheki mtandaoni Evolution Garage kwenye instagram au facebook.
 
Kama issue ni brake pads mbona hapo hakuna ubabaishaji,wape wafungue tairi zote watoe hizo pads ili ujiridhishe na wewe kuwa zimeisha.Ila kwa uzoefu wangu utakapopata fundi sahihi utakuta umeponyesha na vingine ambavyo uliona kama unaliwa hela....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pia kuna garage ipo mbele ya stand ya 8 8..nyuma kdg ya bank ya NMB Uyole..(siikumbuki jina)..ni dealers wa vipuri vyote vya toyota na wana mafundi waziri haswa(hawanaga ubabaishaji)..mm pia niliwah miliki premio ikawa na tatizo flan hv..hangaika mbeya mjini naona mafundi wananilia hela tu..nikaelekezwa na mtu huko..tatizo liliisha siku hyohyo

Hao wanaitwa Mwaji Group ni dealer wa Toyota na wana gereji hapo. Wapo kabla ya Stendi ya 8&8 ukitoka mjini unapokuja Uyole.
 
Back
Top Bottom