Naomba kufahamishwa gereji nzuri na ya kisasa Mwanza

Sambusa kavu

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2015
Posts
806
Reaction score
1,296
Wadau heshima zenu, natumaini mu wazima wa afya na poleni na majukumu ya kulijenga taifa..

Naombeni kufahamishwa gereji nzuri iliyopo mwanza ambayo naweza kwenda kupaka rangi kipasso changu....

Kwasasa nipo shinyanga, bodaboda akapitia kipasso changu milango yote miwili ikakwaruzika..

Nikabugi kupaka rangi hapa hapa shinyanga.... Daaaah gari imetokea kachumbari kabisaaaa... jamaa wameniharibia kabisa yaan bora nisingepaka iyo rangi...

NAAMINI LABDA MWANZA KUTAKUWA NA GEREJI KUBWA NA YA KISASA AMBAO NI MAPROFESSIONAL AMBAO WANAWEZA WAKANIPAKIA RANGI KIPASSO CHANGU KING'AE... WADAU WA MWANZA NAOMBENI MSAADA TAFADHALI....
 
kuna garage ya wachina ipo mwanza kama unaenda nyegez ila nimesahau jina lake boss
 
Nenda kwa Mzee Lymo pale sisi kwa sisi Igogo.

Ukiwa Poa mfukoni nenda kwa MORAF
 
Nenda kwa Mzee Lymo pale sisi kwa sisi Igogo.

Ukiwa Poa mfukoni nenda kwa MORAF
Hao Moraf mkuu ndo wapo sehem gani?

Halafu vip kuhusu ubora wao wa kazi ni mzuri sana kuliko hapo igogo au?... Kama kazi nzuri na ya kuridhisha hata kama wapo expensive kidogo sio ishu
 
Hao Moraf mkuu ndo wapo sehem gani?

Halafu vip kuhusu ubora wao wa kazi ni mzuri sana kuliko hapo igogo au?... Kama kazi nzuri na ya kuridhisha hata kama wapo expensive kidogo sio ishu

MORAF ni pale jirani kabisa na walipokuwa VRAJLARS ni Barabarani tu.
ila kwa jinsi nilivyokuelewa shida yako wewe sio mpaka rangi wa gari , bali ni rangi ya gari yako na atakaye ipaka.

kwa uzoefu wangu mdogo tu hiyo gari ipake rangi inaitwa maroon. namba ya rangi hiyo in depend na VIN ya gari yako.
 
Kwa Mwanza nenda kwa Wachina, waswahili wa gereji za kupaka rangi Mwanza kazi zao siyo nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…