Mkuu kama umetoka nayo Songea to Dar Mbona majibu ya baadhi ya maswali yako hapo juu unatakiwa uwe nayo? Anyway nitakupa abc chache nazofahamu kwa engine.
Nitaongelea engine ya 4D56 turbo common rail DID ya Diesel ambayo mie ndo nina uzoefu nayo.
It’s a very powerful engine, inachanganya haraka sana, very impressive fuel economy (1 liter for 12-14 km on highway na 1 lita kwa km 10 ukiwa mjini). Inapanda milima kama vile ni mteremko na ina pulling ya kuvutia sana.
Engine ina CC 2500 na kwa kweli haisumbui. Nilichoona kama ndo ugonjwa wa hii gari ni clutch, katika miaka 6 niliitumia nimedeal na clutch mara 4 mpaka sasa. Hivo naamini ukipata ya automatic may be utakwepa hilo tatizo.