Naomba kufahamishwa hospitali ya gharama nafuu ambayo naweza kupata vipimo vya afya ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula

Poluyakhtov

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2017
Posts
358
Reaction score
300
Habari za Alasiri wana JF,naomba kufahamishwa hospitali ya gharama nafuu ambayo naweza kupata vipimo tajwa hapo juu katika mkoa wa Dar Es Salaam.

Nataka kufanya check-up hiyo kwa sababu kwa muda mrefu nimekuwa nikikabiliwa na changamoto kadhaa kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

Changamoto zenyewe ni -:

1} Persistent Constipation

Hili tatizo limekuwa likinitokea mara kwa mara licha ya kwamba nakunywa maji mengi sana kwa siku,lakini hutoweka nikitafuna vitunguu Swaumu au kula baadhi ya matunda kama mapapai,Parachichi au Chungwa.

Kwa kawaida huwa napata choo kikubwa kwa wiki mara 3 au 4 tu.


2}Tumbo kunguruma lakini haliumi.

3}Uwepo wa Stone-like objects kwenye choo kikubwa,ingawa hii huwa kwa kiwango kidogo sana na huweza kutokea mara moja kila baada ya miezi kadhaa.


4} Maumivu ya mgongo upande wa juu wa kulia.

5}Kuhisi kushiba hata kama nikila chakula kidogo.

6}Uwepo wa stiff skin tags eneo la njia ya haja kubwa pindi ninapojisafisha
.Ingawa nikigusa tu hupotea au mara nyingine hauonekani kabisa.

7}Kuna wakati nilikuwa napata maumivu katikati ya kifua,kitu kama acid reflux,na nilipofuata ushauri wa forums mbalimbali za afya kama kutokulalia mgongo baada ya kula,tatizo hilo lilipotea.

Naomba kufahamishwa juu ya hospitali ninayoweza kupata huduma nafuu kwa matatizo hayo.




Pia kuna kipindi nakuwa na mawazo makali sana kama depression au anxiety.Je,inaweza kuwa sababu mojawapo?


Siku njema.
 
Nenda hindumandal dsm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…