Naomba kufahamishwa kwa undani kuhusu unenepeshaji wa n'gombe

Naomba kufahamishwa kwa undani kuhusu unenepeshaji wa n'gombe

mwenye shamba

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
978
Reaction score
1,766
Waungwana salaam!

Napenda kufahamu kwa undani kuhusu unenepeshaji wa ng'ombe.

1. Mchanganyiko wa chakula

2. Kiasi anachokula ng'ombe kwa siku

3. Nyasi ale kiasi gani au asile kabisa?

4. Ili asizidishe gharama za uendeshaji auzwe muda gani tangu kuanza kunenepeshwa?
 
Jibu no 1. Tumia mchanganyiko hue na pumba za mahindi, mashudu ya pamba au alizeti (pamba ni mazuri zaidi kwenye kunenepesha ),na madini(ya dukani pamoja na chokaa au dcp au mifupa na chumvi ya mezani)
 
Jibu no 4. anenepeshwe kwa miezi 3. Huu mda unamtosha kurecover uzito aloupoteza kipindi hiki cha kiangazi na kuongezeka zaidi ila pia faida inapatikana.
 
Tafta azolla af shudu kiaina

Nyasi fanya kuzikatakata na uzilowanishe kwa maji ya chumvi ya magadi kisha mpe ng'ombe.

Mwzi mmoja tu utakuja PM
 
Gharama ya matumizi ya azolla ni bei gan kwa mwezi? Ni kwel ndani ya mwezi mmoja mnyama anakua kashanenepa kutoka kwenye kukondeana ili kwenda sokoni?

Tafta azolla af shudu kiaina
Nyasi fanya kuzikatakata na uzilowanishe kwa maji ya chumvi ya magadi kisha mpe ng'ombe.
Mwzi mmoja tu utakuja PM
 
Mimi pia napenda sana hii biashara,ila natafta mzoefu anaefanya nimtembelee shamban kwake nikaone practically
 
Waungwana salaam!

Napenda kufahamu kwa undani kuhusu unenepeshaji wa ng'ombe.

1.mchanganyiko wa chakula

2.kiasi anachokula ng'ombe kwa siku

3.nyasi ale kiasi gani au asile kabisa?

4.ili asizidishe gharama za uendeshaji auzwe muda gani tangu kuanza kunenepeshwa?
Hii ni biashara kama biashara nyingine. Swali langu kwako,ni kwanini umeamua kuingia kwenye hii biashara?
 
Kuchanganya chakula kwenye kilo 100
Pumba 70%
Mashudu 25%
Mineral-2.5
Salt-2.5
Pia kama wanagraze au unawakatia majani wakati wa mchana
Kunenepesha ni miezi mitatu hadi minne

Pia kingine cha kuzingatia ng'ombe awe mkubwa kwa umri na asiwe ndama
Asante kwa mchanganuo huu. Naomba kujua quantity gani anapatiwa kila ngombe kwa siku?
 
Back
Top Bottom