Salaam ndugu,
Najaribu kukueleza kwa ufupi hapa:
Juzuu maana yake halisi ni "sehemu") ni moja ya sehemu thelathini za urefu tofauti ambapo Quran imegawanywa.
Quran ni maandiko makuu ya dini ya Kiislamu, yanayoaminiwa na Waislamu kuwa ni ufunuo kutoka kwa Mungu. Quran imepangwa katika sura 114 na Juzuu 30
ULAMAA: Ni wajuzi wa uislamu, ambao wamehusishwa na uchambuzi wa hukmu za kiislamu, na wakaasisi kwa ajili kudhibiti misingi ya halali na haram, na wao katika ardhi nafasi yao ni kama nyota katika mbingu, kupitia wao huongoka waliopotea katika viza, na haja ya watu kwao ni zaidi ya haja yao kwenye chakula na kinywaji.
Msahafu, kitabu kitakatifu cha kislamu. Kimeundwa na Juzuu 30 na sura 114