Naomba kufahamishwa machache kuhusu Chuo cha Wanyamapori Pasiansi

Naomba kufahamishwa machache kuhusu Chuo cha Wanyamapori Pasiansi

Political stability

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
906
Reaction score
1,401
Wakuu habari za mihangaiko..

Nilikuwa naomba, kujuzwa vitu vifuatavyo kuhusu chuo cha wanyapori , Pasiansi wildlife, kilichopo Mwanza.

1. Sifa za kujiunga na hicho chuo
2. Kozi zitolewazo
3. Kozi ni za muda gani
4. Gharama (ada)
5. Na baada ya kuhitimu, upatikanaji wa ajira upoje

NB: Nimejaribu kutembelea kwenye website, there something went wrong.
 
Ada ni million mbili laki nane kwa course ya Basic certificate in wildlife management and law enforcement na million tatu kwa course ya technician certificate in wildlife management and law enforcement kozi zote ni mwaka moja Ila kwa upande wa basic sifa ni uwe na pass kwenye masomo ya biology na geography na kwa upande wa technician certificate sifa uwe ni form six na uwe na pass mbili kwenye masomo yako au uwe na cheti cha basic.
 
Kwa basic na technian huwa hawatofautiani.

Sana scale ya salary hata wakiajiriwa tofauti huwa ni shillingi elfu kumi hadi ishirini inategemeaana na taasisi uliyoajiriwa Kama ni tawa au tanapa au ngorongoro au halmashauri ila majukumu yao kazini wote ni Sawaa.
 
Ajira zao siyo ngumu Sana mwanafunzi akimaliza anaweza kusubiri ajira lakini sidhani Kama atakaa zaidi ya miaka mitatu nyumbani ingawa wengine wanamaliza na kuajiriwa baada ya mda mfupi tu inategemeaana na bahati ya mtu mwenyewe.
 
Hawa jamaa wakiajiriwa mishahara yao ni mizuri Sana fikiria mtu anamaliza form four anaenda anapiga zake mwaka moja anaajiriwa tanapa au ngorongoro anaanza na mshahara wa million moja na laki mbili na bado anapewa posho ya Doria kila mwezi.
 
Hawa jamaa wakiajiriwa mishahara yao ni mizuri Sana fikiria mtu anamaliza form four anaenda anapiga zake mwaka moja anaajiriwa tanapa au ngorongoro anaanza na mshahara wa million moja na laki mbili na bado anapewa posho ya Doria kila mwezi.
Dah aisee safi, sema ada yao, imesimama
 
Back
Top Bottom