Wakuu Kwema?
Nahitahi kumfungulia mtu Biashara ya Kufuga Kuku wa Kisasa, ambapo kwa Kuanzia tumekubaliana kwanza aanze na Box moja. Sasa nilikua naomba mchahngahnuo wa kimahesabu juu ya gharama za kuwafuga hawa Kuku 100....
Mpemdwa pole na majukumu.
Napenda kukueleza kuwa anza ha hao hao 100 kutegemea na nguvu yako, kununua siyo shida shida ni kuwahudumia.
Mimi nilianza na saso hao ni wa mayai.
Vifaa: hakikisha umeandaa sehemu ya kulia chakula ambayo inaweza ikawa mbao iliyotengenezwa au vyombo vya kisasa ambavyo itabidi viwe si chini ya 7
Halafu vyombo vya kunywea maji unaweza nunua kama 2, au tatu kama hauko vizuri kifedha toboa hata madumu weka maji watakunjwa vizuri.
Wiki moja unawapa dawa inayonywewa ndani ya masaa matatu then unamwaga maji
Chakula mimi ni chanjo hii ni . 7,000/=
Baada ya mwezi unawachanja tena ile chanjo ya mbavuni dawa huwa ni 15,000.
Chakula wili ya kwanza nunua silverland starter nunua magunua mawili gunia moja ni 64,000/= baada ya hapo nunua grower bei ni kama zinalingana hutaamini wakiwa na miezi mitatu wanakuwa na uzito zaidi ya kilo 2.
Mimi huwa nauza kuanzia mwezi anayetaka nampa wa mwezi, ninao wa intake kama nne anayetaka wa miezi miwili nampa mitatu nampa na sijaona hasara yoyote.
Usichukue wengi kwa kuanza maana wanakula sanaaaaaaaaa unaweza ukakwama njiani
Asante kwa uzoefu wangu nilionao.
Ukiona vipi anza hata wa kienyeji anza na hata 10 tatakuzalia utakuwa mtu mwingine baada ya mwaka
Lakini ukiweza hata wa kienyeji wape chakula mchanganyiko usiwapo pumba tupu hapana hawatakua haraka.
Asante.
Rubelina meena - nafuga kuku