Naomba kufahamishwa, taratibu za kujitambulisha na kutoa kishika uchumba ukweni

Naomba kufahamishwa, taratibu za kujitambulisha na kutoa kishika uchumba ukweni

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Wakuu, poleni na majukumu ya kutafuta Maisha.

Mimi ni kidume, pia staki kabisa kuishi maisha ya kihuni yasiyo na baraka kutoka pande zote mbili, maisha ya kuishi na bibie wangu pasipo kufuata utaratibu maalumu.

Kama thread inavyosomeka hapo, nahitaji kujua na kujiridhisha kwa kina juu ya utaratibu wa kufika ukweni kutambulika na kupeleka kishika uchumba. Binafsi nakiri Nina ugeni kidogo juu ya Jambo hili, pia bi mdogo nae ana ugeni, nlimwambia amdodose Mama mkwe but bado hajanipa mrejesho.

Naombeni mawazo yenu, na uzoefu wenu wadau.
 
Ina maana huko kwenu huna ndugu watu wazima, au ndo ule uchumba wa Instagram?!
Npo mbali na home na Wala siishi home! mzee wangu ashatangulia mbele za haki muda mrefu Sana, nlimweleza mother akaniambia hayo nifanye mwenyewe maana kimila yeye haruhusiwi!

Kuuliza sio ujinga, Nataka nijazie mambo yaende vzur!
 
Jua kabila la binti na miiko yao.....

Kaa chini na mshenga wako akatafiti familia ya binti vizuri (taratibu zao za kuolewa zipoje na mahali au kishika uchumba kinakuwaje

tafuta mshenga ambae ni kabila moja na binti.....

jitahidi upate washenga waongeaji na wacheshi

Jiandae na swali juu ya siku ya kuoa....maana ukweni kabla hawajapokea kishika uchumba huwa wanataka jua umejipangaje kuhusu steps zijazo

Anza kufanya mawasiliano madogo na wakwe zako....mfano kusalimia kwa simu mama. Wajomba. Bibi. Babu. Baba etc ili uzoeane nao usipate shida ya mamahari makubwaa....

Lamuhimu sana hapo juu ni kutafuta mshenga ambae ni ama kabila la binti au anaijua familia ya binti vizuri na wanajuana etc
 
Wakuu, poleni na majukumu ya kutafuta Maisha.

Mimi ni kidume, pia staki kabisa kuishi maisha ya kihuni yasiyo na baraka kutoka pande zote mbili, maisha ya kuishi na bibie wangu pasipo kufuata utaratibu maalumu.
Una umri gani mpaka usijuwe sheria za ukweni kwenu?
 
Washirikishe Baba zako wakubwa na wadogo, mashangazi kwa vyovyote watakupatia ushirikiano, kila lakheri.
 
Kwanza kabisa Kama umesema wewe siyo muhuni basi utakuwa unaingia kanisani mtafute mzee wakanisa au mtu mzima yeyote anaesali kanisani kwenu ..

Hawa watu hujua taratibu nyingi zakimila kitamaduni pia nazakidini Kama huna ushirika wowote kanisani ..

Tafuta mtu mzima yeyote wakabila la mchumba wako akupe muongozo af tafuta mtumzima pia yeyote wakabila lako nae akupe utaratibu wakwenu ..

Kisha peleka taharifa ya ugeni ukweni ..alaf andaa mshenga mahana taratib nyingi na mazungumzo hufanywa na washenga ivyo wew utakuw beki tu ... Usiogope .. Ni simple .. ..
 
Inshort tafuta mtu Muongeaji anaejitambua anaenda kufanya nini na anae weza kujibu maswali vizuri maana siku hiyo wewe utakua kimnya kabisa.. , pia kua na hela kiasi isiyo pungua milioni moja na uwe na tarehe maalum ya kufunga ndoa hata kama itakuja kubadilika mwishoni ila uwe umejipanga ukiulizwa ujibu vyema.. kama pia mtataka kuvalisha pete ya uchumba jiandae na siku utakayo waambia ni lini
 
Npo mbali na home na Wala siishi home! mzee wangu ashatangulia mbele za haki muda mrefu Sana, nlimweleza mother akaniambia hayo nifanye mwenyewe maana kimila yeye haruhusiwi!

Kuuliza sio ujinga, Nataka nijazie mambo yaende vzur!
Tayari mama yako amekupa muongozo: kimila mama haruhusiwi. Mrudie umuulize kama mama haruhusiwi, ni nani anayeruhusiwa? Utakuwa umepata pa kuanzia.
 
Mkuu tafta mshenga, ni kipengele sana kama unataka kupewa hati halafu mshenga huna! Mshenga awe kabila la binti na aijue lugha ya nyumbani kwao pia awe mchangamfu akiwa mzembe atakula fine🤣!

Mshenga wako na msemaji wao wa familia watamaliza shughuli kwa wepesi kabisa! Mwambie binti atafute msemaji wa familia yao aidha mzee wake au kaka mkubwa!
 
Back
Top Bottom