Ni zao jamii ya mikunde,hali hitaji mvua wala maji,linahitaji ardhi yenye unyevu nyevu wa kuweza kuotesha tuu wakati wa kupanda ili iweze ku germinate,hupigwa dawa kwa ajili ya wadudu waharibifu mara 1 mpaka 3 kutegemeana na wadudu husika(dawa hupigwa kuanzia week ya 2 baada ya kuota katika shina),huota kwenye mwinuko wowote kuanzia 0-2400m kutoka usawa wa bahari na ardhi iliyopata mvua kuanzia 750mm+ kwa mwaka,mara nyingi maeneo yenye irrigation wakishatoa mazao ya mwanzo hufaa sana (eg mashamba ya mpunga).
Huchukua siku 60-70 kuanza kuzaa(pods) na siku 90 kuanza kukauka,mpka kuvuna huweza kufika mpaka siku 150+.(hapa hutegemea kama ardhi ilikua mbichi sana hua haizai/kutoa maua mapema,wakati mwingine kama ikipata maji zaidi sumu ya kuua majani kidogo hutumika ili kuilazimisha pods zikomae mapema),wakati mwingine unaweza vuna mvuno wa kwanza unaipa unyevu kidogo tena itazaa tena mara ya 2.
Ekari moja ya 4900m² huzaa kutokana na timing ya upandaji na matunzo na huweza kutoa gunia mpka 10(matunzo mazuri sana),ila mara nyingi kibongo bongo hua ni 4-8(gunia lina kilo 100).
Bei hutegemeana na soko la wakati huo inaweza fika mpaka 4000tzs kwa kilo moja.
Kwa sasa kilo ni 3000tzs ila tunapo elekea itafika 5000tzs.
Maeneo mazuri ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Mbeya na maeneo yanayoyazunguka mikoa hii.
Gharama:
Shamba @50,000/=
Sumu ya kuua majani(badala ya kuingiza trekta) @12,000/=
Kupiga dawa bomba 2@5,000
Maziwa ya wapiga dawa 2
Lita 2
Pump utakodi 2 @3000
Kupanda @30000
OR
Ukilima kwa trekta @40,000/=
Kupanda nyuma ya trekta @5000
OR
Kupanda kwa jembe @25,000
NB:Nnavyo changia uzi huu nipo shambani napambana na eka 50 katika mkoa wa Manyara,Babati,kijiji cha Magugu
Kuna kampuni walitaka Tani 2000(kilo 2,000,000) na sijui kama itapatkana tena kwa bei mtayokaa mezani..
Una swali uliza hapa hapa