Naomba kufahamu dawa ya kuzuia NDEVU kuota haraka

Mdau jf

Senior Member
Joined
Sep 10, 2020
Posts
182
Reaction score
313
Bandugu nina wahi sana kuota ndevu na masharubu(timba) yaani nikinyoa hazipi siku tano yashajaa tena haswa haswa hizi timba ndiyo kero kabisa.

Nikisema nikae mwezi bila kunyoa unaweza sema muisrael.

Kwa yeyote anaye fahamu dawa ya kuzuia ndevu kuota kwa haraka ama kuzuia zisiote kabisa anifahamishe.
 
Mkuu ndevu ndo uanaume
 
Ngoja waje wataalama wa dawa ya kuzuia ndevu.
Ila mchebe ukiuchonga vizuri alafu ukaupiga mafuta yake unakuwa na muonekano mzuri,mwanaume kuwa na ndevu ni kawaida.
 
Ndevu si mzigo mkuu
 
Demu wangu hapa anasema kwa kucheka kwanini usiwe shoga tu.
 
Dawa za kuzuia nywele kuota zipo nyingi sana na brand tafauti tafauti; nakushauri kama unaishi kwenye miji mikubwa kama Dar au Arusha tembelea maduka makubwa ya cosmetics watakushauri dawa nzuri kutumia kutokana na ngozi yako umri n.k.
 
Upo sahihi,kama kila baada ya siku mbili unanyoa ndevu mashavuni ina maana hazina kazi,ni bora zisiote uache za kidevuni tu,inasaidia kutunza ngozi na kupunguza usumbufu

Wafatute wamasai wana hizo dawa mkuu,ila hakikisha awe ana kijiwe ambacho anakuwepo kila siku, hao wanakuwa sio matapeli
 
wadada wanasuka mara moja kwa shilingi elfu hamsini , mwanaume kunyoa mara nne kwa mwezi kwa shilingi buku mbilimbili unaona tabu kweli? ndevu zinategemea na genetics na homone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…