david Junior
New Member
- Dec 30, 2017
- 3
- 0
Habarini... naomba kufahamu jinsi ya kutengeza yorghut kwa yeyote mwenye uzoefu nayo....asante.
------
------
Wengine kiingereza hatujui mkuu. Yoghurt ndio mtindi?
Kama ndio basi fanya hivi...
Andaa vifuatavyo;
Maziwa ya maji kiasi upendacho
Mtindi kiasi
Sufuria safi
Chujio
Chombo cha kuhifadhia maziwa kisafi chenye mfuniko
Chemsha maziwa yako vizuri kabisa, yaache yapoe, yakipoa yachuje ili kuondoa ule utando wa juu.
Kisha changanya na mtindi (lita tano ya maziwa weka glass moja ya mtindi) yakoroge vizuri yachanganyikane, kisha funika vizuri weka sehemu safi.
Baada ya masaa kumi na mbili mtindi wako utakuwa tayari, koroga vizuri na tayari kwa matumizi.
Ziada: lita tano ya maziwa inawekwa glass moja ya mtindi, hivyo ikiwa chini ya hapo jitahidi kukadiria.
Wenye ujuzi zaidi watatujuza.