Naomba kufahamu kuhusu Bima za magari

Naomba kufahamu kuhusu Bima za magari

Anete Insurance Agency
Wapo Urafiki Karibu na kutuo cha police tunatoa huduma zote za bima mahali popote ulipo Tuwasiliane kwa namba 0713613891
 
Naomba anaejua kuhusu bima za magar zinagharimu sh ngap, mud a gani,je zinatofautianaje na zile bima za nyumba.?
Kwanza Bima za magari zipo za aina mbili Kuna Bima kubwa (comprehensive) Na Bima Ndogo(third party), Ya kwanza ina ghrama kubwa kwa sababu hii inalinda risks zote pamoja na gari lenyewe , na ya pili ni kwa ajili ya mtu yeyote atakaye athirika kutokana na matumizi yako ya gari kama vile mtembea barabarani uliye mgonga n.k Hivyo ukikata bima hii ndogo, gari lako linakuwa halilindwi bali ni kwa ajili ya lawama zatakazotokea.
Na kuhusu gharama, hakuna kiwango kamili kabisa, ila kinatofautiana kulingana na makampuni ya Bima, Thamani ya Gari lako(sum insured), aina ya cover unayokata(kama nilivyoainisha hapo juu), Matumizi ya hili gari lako kama ni biashara au private!
 
Halafu hawa watu wa Bima mbona hawaweki gharama zao wazi...!?
 
Back
Top Bottom