Naomba Kufahamu ni Kipi Kinawafanya Wachezaji wa Kigeni Kupenda Kucheza Soka Tanzania?

Naomba Kufahamu ni Kipi Kinawafanya Wachezaji wa Kigeni Kupenda Kucheza Soka Tanzania?

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Japo mimi sio mfatiliaji sana wa mpira wa miguu ila nimekiwa nikijiuliza hili swali.

Ni kitu gani kinawafanya wachezaji wa kigeni kupenda kucheza soka la kulipwa Tanzania?
  • Je, wanapata mshahara mzuri?
  • Je, wanapewa mahitaji ya msingi kama nyumba na magari na bonasi nyingi?
  • Je, starehe zipo za kutosha?
  • je watanzania wanapenda sana mpira kiasi kwamba mchezaji? anajisikia kupata sapoti wakati wote?

Binafsi sifahamu. Nimekuwa nikisoma magezeti mbalimbali yaani unaona wapo wachezaji huku nje tamaa yao ni kucheza Tanzania. Yaani Tanzania hii hii ambayo sio nchi tajiri, inanishangaza sana.

Nitatoa mifano michache,

Unasikia mchezaji kama Okwi anatamani kurudi kucheza huku. Yule Makambo alirudi kucheza tena huku. Kuna mchezaji wa Rwanda Tuyisenge alipohojiwa anasema anaamini kama deal litaenda vzr siku moja atakuja kucheza bongo.

CEO wa Simba majuzi anasema anapata simu za mawakala wengi wachezaji wao wanataka kuna kucheza Tanzania Simba etc.

Ndugu yangu mmoja aliniambia kuna wachezaji fulani wa kigeni baada ya kustafu soka sasa wanaishi bongo.

Sasa niwaulize nyie mnaojua soka la bongo, kipi kinawavutia wageni kucheza hapa? Kiasi kwamba mchezaji yupo radhi hata kucheza ligi daraja la kwanza!!
 
Mapokezi walioyafanya Yanga Kwa Eng. Hersi, Carlinhos n.k huenda yamewavutia.

League yetu inazidi kujipatia maarufu na inazidi kupata exposure. Wanaamini itakuwa ni daraja la kuwavusha kuwapeleka mbali zaidi.
 
Ligi ya Tanzania kwa ujumla Vilabu vyake vinalipa maslahi mazuri zaidi kuliko nchi yoyote ktk ukanda huu wa East and Central Africa kuanzia maslahi kwa wachezaji mpaka makocha

Hata ukiangalia kwa miaka hii kumi mfululizo hakuna top player yoyote ktk ligi yetu aliyesajiliwa kwenda ligi ktk nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi wala Msumbiji isipokuwa Congo DRC team kama Tp Mazembe labda na As Vita ndio vina msuli wa kuchukua mchezaji top player ktk ligi yetu.

Na kudhihirisha hilo zaidi ndio maana timu zetu za bongo hasa Simba, Yanga na Azam zina uwezo wa juu kabisa wa kusajili top player yoyote ktk ligi ya nchi zinazotuzunguka isipokuwa kwa Congo DRC tu tena kwa ni kwa Tp Mazembe tu.

Simba walishamsajili Kahata aliyekuwa MVP ligi ya Kenya, Dodoma jiji timu level ya kawaida kabisa lakn walimsajili Dickson Ambundo kutoka Gor Mahia Kenya, Azam walimnyakua kipa David Kisu kutoka Gor Mahia

Imagine wachezaji kama Deo Kanda, Amis Tambwe wapo timu ya daraja la kwanza nchini

Pia sababu nyingne ni udhamini mnono unaozidi kupata thamani kila mwaka ktk ligi yetu unaifanya kuzidi kuvutia foreign players wengi kutamani kuja kucheza kwetu

Na hili haliwavutii wachezaji tu ni mpaka Makocha wa kigeni wanamiminika ktk ligi yetu
 
Mishahara yao haikatwi Kodi, ukimaliza mkataba unapotaka kuongeza unalipwa Tena fedha ya kusajili, maisha ya bongo ninafuu kwakua buku unakula ugali ukashiba, unaweza kuishi bila kibali Cha kufanya kazi na usibugudhiwe labda uharibu mwenyewe.

viongozi wa Klabu Wana mbinu chafu nyingi za kuisaidia timu ishinde kwaiyo inawapa wachezaji unafuu katika uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom