Honda ni gari nzuri sana, nakumbuka ni my first car Honda Accord series ya mwaka 1985 yani ilikuwa inanizidi umri from the year of manufacture. Sasa kimbembe ni spare parts zake kama suspensions, engine parts na vinginevyo, kwa general service naona shida kwenye filters na aircleaners.
Ni gari inayivumulia mikikimikiki sana. kinachofanya iwe gharama kuihudumia ni Spares zake kutokupatikana maeneo mengi hapa nchini. Ila kwa CRV naona zipo nyingi tuu na parts zake zinapatikana pale ilala za kutosha sana, bei zake ni za kawaida hata vitz spare zake ni aghali kuliko hiyo CRV.
Kitu cha kuzingatia ,lazima ujue unanunua gari ajili ya matumizi gani. Usije nunua IST ukitegemea uipeleke shamba.