Kiswahili ni lugha ya kibantu
Hapana siondiyo. nasikia kuwa baadhi ya wazanzibari wanaelewa kiswahili kama hicho, hata nembo ya Chuo Kikuu cha Zanzibar ina herufi hizo. Je, huku kuna mzee mzanzibari anayeweza kunisaidia?
View attachment 1681760
Asante sana bwana, unachoelezea ni ya kweli kabisa.Bakari, Kiswahili sio lugha ya kibantu pekee, Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha kadhaa kama, 1- kibantu (lugha za makabila ya wabantu), 2- Kiarabu, 3- Kireno, 4- kijerumani, 5- kihindi.
Katika kiswahili, Kibantu ni takriban maneno 70%, kiarabu 25%, na 5% ni hizo lugha zingine.
Kwa maneno mengine kiswahili ni lugha chotara (hibreed language/ clone language).
Hicho ni kiarabu sio kiswahili japo inawezekana kuandika kiswahili kwa kutumia herufi za kiarabu mfano hapo chini kwenye picha inasomeka "Bakari anakula nanasi"View attachment 1682485
Kama hakikuwa na kibantu sio kiswahili kamilikatika sehemu za pwani hassan Unguja na Lamu, hata leo baadhi ya watu hutumia alama hizo za kiarabu kuandika kiswahili.
Marehem baba yangu alikuwa anajua kuandika aina zote mbili kwa kuwa babu yangu hakuwa akitumia hati za Kilatini, kwa hiyo walikuwa wakiandikiana barua za Kiswahili kwa hati za kiarabu, ila mimi nilikuwa tunaandikiana kwa hati za Kilatini. Sahihi usemavyo, ila 90% ya watu hawajui kitu hichi, alipokirasimisha Muingereza Kiswahili mnamo miaka ya 1930 hivi , akachagua Kiunguja Mjini iwe lahaja rasmi ya Kiswahili dhidi ya lahaja ya Kimvita (Kimombasa), na akakifanya kuwa na hati za Kilatini kutoka za kiarabu.katika sehemu za pwani hassan Unguja na Lamu, hata leo baadhi ya watu hutumia alama hizo za kiarabu kuandika kiswahili.
Hata maeneo ya kwetu Rufiji, maana nakumbuka wakati tupo Madrasa mwalimu wetu alikua anatufundisha kuandika kiswahili kwa herufi za kiarabu. Kama kuandika Barua ya uchumba.katika sehemu za pwani hassan Unguja na Lamu, hata leo baadhi ya watu hutumia alama hizo za kiarabu kuandika kiswahili.
alipokirasimisha Muingereza Kiswahili
Ni aina ngapi ya maelezo unayajua ?🤣 Hiyo ni "syntax" ya kiarabu!!, katika Kiswahili ilitakiwa iwe hivi:-
"---Muingereza aliporasimisha kiswahili---".
kinakuwa mkuu. maneno mengi ya kiswahilo yanatokana na kiarabu sasa hujiulizi hao waarabu wanaandikajeDaah labda sijaelewa yani kiswahili chenye herufi za kiarabu ? Sasa Hapo kinakuaje kiswahili tena?
Acha ujinga na ujuajiHiyo ni Quran, na sio kitabu cha kiswahili hicho.