Naomba kufundishwa ufundi simu

Naomba kufundishwa ufundi simu

Mdugo

Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
55
Reaction score
37
Salaam wana jukwaa.

Naomba nianze moja kwa moja bila kupoteza muda. Mimi ni mhitimu wa Chuo cha Kikatoliki Mwenge, Moshi katika Bachelor of Science With Education. Katika pita pita zangu nimefundisha shule kadhaa tangu nimalize mwaka jana, Ila naomba kupata ujuzi zaidi katika Ufundi wa Simu.

Interest yangu ni kuwa Fundi wa Hardware pamoja na Software katika simu. Naomba kama kuna Fundi tayari katika Forum hii, Anisaidie mawazo na Jinsi navoweza kujifunza skills hizi za ufundi.

Pia, kama anaweza kunichukua nikawa namsaidia kazi zake huku nikiwa najifunza kwake, kama masomo ya mafunzo kwa vitendo itakuwa vizuri zaidi maana nitajifunza vizuri na kwa ufasaha zaidi.

Asante, Nawasilisha.
 
Veta kipawa wametangaza nafasi 400 kwa wote wanaohitaji kujifunza fani ya ufundi simu. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 mwezi wa 7 mwaka 2020, tembelea website yao au veta kupata taarifa zaidi. Mafunzo yanagharamiwa na Serikali.
 
*TANGAZO*
*Mkuu wa CHUO CHA TEHAMA CHA VETA KIPAWA anakutangazia nafasi ya kusoma kozi Maalum ya Ufundi simu kwa muda wa Wiki 6. Mafunzo haya yatawanufaisha washiriki 400 kwa ufadhili wa ADA pekee toka Serikalini.*

Mafunzo haya yatakuwezesha mwanafunzi kusoma hatua zote tatu za mafunzo yaani;
1. Hatua ya Awali *(BASIC)*
2. Hatua ya Kati *(INTERMEDIATE)*
3. Hatua ya Juu *(ADVANCE)*

Utakapofaulu na Kuhitimu, utatunukiwa *CHETI* kutoka *VETA* kitakachokuwezesha kupata *LESENI* kutoka *Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)* inayokupa kibali kufanya kazi ya ufundi Simu.

Mafunzo haya yatakuwezesha kufahamu na kupata ujuzi juu ya;
1. *Misingi ya utengenezaji wa vifaa vya kielekitroniki*
2. *Kutambua na kutatua matatizo ya simu za mikononi (SOFTWARE & HARDWARE)*
3. *Elimu ya Ujasiliamali*
4. *Utambuzi wa Sheria, taratibu na kanuni za Mawasiliano zinazoongoza tasnia nzima ya ufundi wa Simu*

*Mafunzo haya ni BURE. Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 15/7/2020*

Huu ni ufadhili unaotolewa na *Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania* kupitia *Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)* chini ya *Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).*

Fomu za maombi ya ufadhili zinapatikana kupitia http://tiny.cc/ufundiSimu au Tembelea tovuti ya Chuo www.vetakipawa.ac.tz

Mafunzo yatafanyika katika chuo cha TEHAMA cha VETA KIPAWA kilichopo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Ilala, Kata ya Kipawa (Karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere.

*Kwa maelezo zaidi Piga simu 0714 720 381*

*IMETOLEWA NA MKUU WA CHUO CHA TEHAMA VETA CHA KIPAWA*

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
*TANGAZO*
*Mkuu wa CHUO CHA TEHAMA CHA VETA KIPAWA anakutangazia nafasi ya kusoma kozi Maalum ya Ufundi simu kwa muda wa Wiki 6. Mafunzo haya yatawanufaisha washiriki 400 kwa ufadhili wa ADA pekee toka Serikalini.*

Mafunzo haya yatakuwezesha mwanafunzi kusoma hatua zote tatu za mafunzo yaani;
1. Hatua ya Awali *(BASIC)*
2. Hatua ya Kati *(INTERMEDIATE)
Asante sana... Ngoja nijisajili.

Haya mafunzo ni kwa ajili ya sheria na taratibu za TCRA katika ufanyaji kazi. Pia nadhani ni maalum kwa ajili ya kupewa leseni na kutambulika.

Asante sana kwa kunipa hizo taarifa sikuwa nazo kabisa.
 
Back
Top Bottom