mama dunia
JF-Expert Member
- Dec 22, 2011
- 420
- 84
Jamani nipeni tips za kuupika mhogo upikike utest nicely nienjoy nawapendwa wangu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Muhogo wa nazi wa kukaanga au kuchemsha?
Siri ya muhogo pia ni muhogo wenyewe...kuna muhogo ukiupika mara moja ila mwengine hata uutie nazi ngapi utakuta unakuangalia km ulivyokua
hii ftari yangu ya kesho, asante sana, kiukweli muhogo kwangu mwenzie samaki. vp itaenda vizuri?Mie binafsi ninavyopika ni hivi,
Mahitaji
-mihogo
-nyama/maharage
-nyanya
-kitunguu maji kikubwa
-karoti
-pilipili hoho
-pilipili mbuzi
- tui zito la nazi,
-chumvi
-mafuta
maandalizi,
osha vitu vyako vyote kwa maji safi na salama,
-mihogo imenye kisha ikate katika vipande(napendelea vibox)ili iwive haraka.
Njia ya kwanza,
unaweza kuchemsha mihogo na kutia viungo vyote,
AU unaweza kuchemsha mihogo na nyama ikishaiva,unakaanga viungo kisha unatia mihogo na nyama unachanganya,na mwisho unatia nazi,
n.b chumvii ni muhimu kuweka kwenye mihogo wakati unachemsha,
pia kama haupendi ukali wapilipili mbuzi unaweza kuiosha na kuidumbukiza bila kupasua.
Mie binafsi ninavyopika ni hivi,