Naomba kujua aina za Engine na tabia zake

Naomba kujua aina za Engine na tabia zake

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
1,845
Reaction score
2,248
Wakuu kwema humu?
Naomba kujua aina zote za engine za magari na tabia zake.
Mfano gx 100 mara 3l, mara 2R sijui nini yani natamani sana kujua wakuu.
Wekeni tu nyingi iwezekanavyo tupate shule.

Mbarikiwe sana.
 
Ungekua specific, kidogo. Kuna aina za magari zaidi ya Elfu kadhaa. Mfano Toyota, Nissan, Mercedes Benz, BMW, Volkswagen etc.

Ungesema mfano engine za Magari ya Toyota. Tena kua more specific sema Model fulani ya Toyota mfano Corolla.

Hapo tutaenda sawa somo lisiwe refu sana.

Wewe unataka engine ya gari gani model gani?
 
Swali lako lina majibu mengi hata sijui unataka lipi mfano 1.Aina ya engine kulingana na nishati inayotumika (i)petrol engine (ii)diesel engine (iii)natural gas engine. 2.Aina ya engine kulingana na upozaji (i)water cooling engine (ii)air cooling engine. 3.Aina za engine kulingana na mpangilio wa silinda (i) inline vertical (ii)horizontal (iii) horizontal opposed (iv) v-type (v) radially. 4. Aina za engine kulingana na inavyofanya kazi (i)piston engine (ii)rotary engine (iii)turbine engine. Kuhusu alphabet zinazotambulisha engine kama 3L 2R hizi huwekwa na muundaji wa gari ili kukusaidia kununua spare ukifika dukani unasema nataka piston ya 3L unapewa bila kudaiwa sample ( mfano)
 
4s ni engine ngumu sana inapatikana kwenye gari kama mark 11 za kitambo ni nzuri sana saizi zipo kwenye Noah izi engine ni ngumu balaa mafuta zinakuls kidogo sana inaweza kula mpaka km 15 kwa lita kama haijaguswa na mafundi 3L ni engine nzuri pia zna tatizo la kuchemsha
 
Sorry vp kuhusu engine ya carina si 7A sifa yake ni ipi
 
size_does_matter_640_03.jpg
Strange-And-Unusual-Pictures023.jpg
 
4s ni engine ngumu sana inapatikana kwenye gari kama mark 11 za kitambo ni nzuri sana saizi zipo kwenye Noah izi engine ni ngumu balaa mafuta zinakuls kidogo sana inaweza kula mpaka km 15 kwa lita kama haijaguswa na mafundi 3L ni engine nzuri pia zna tatizo la kuchemsha
2L ina sifa zipi?
 
Ku engine kama
Vehicle engines na Search engines kwenye search engine kuna
Yahoo search
Google search
 
4s ni engine ngumu sana inapatikana kwenye gari kama mark 11 za kitambo ni nzuri sana saizi zipo kwenye Noah izi engine ni ngumu balaa mafuta zinakuls kidogo sana inaweza kula mpaka km 15 kwa lita kama haijaguswa na mafundi 3L ni engine nzuri pia zna tatizo la kuchemsha
Hapana umeongea vitu viwili tofauti kidogo mark 2 za zamani zinatumia 1G kavu na 3S iko kwenye noah za zamani pamoja na rav 4 za zamani na ulaji wake wa mafuta hasa 1G inakula sbb ni 6 cylinders
 
Mh hiyo 7A mkuu sina uhakika kama zinafika km 18 kwa lita labda kama umanisha aina ya ti nayo ni km 14 kwa lita so 7A ni kama km 10 kwa lita
Tosha sana hiyo, yaani hata 2km kwa lita tosha
 
Hapana umeongea vitu viwili tofauti kidogo mark 2 za zamani zinatumia 1G kavu na 3S iko kwenye noah za zamani pamoja na rav 4 za zamani na ulaji wake wa mafuta hasa 1G inakula sbb ni 6 cylinders
huwez sema mark 2 ya zamani ina 1G kavu ...mark au gari zingne zina injini nyingi ( option) mfano kwenye mark 2 ya 98 ina ijz gte sasa ww sijui unasema ipi !!
 
Naomba kujua tofauti ya engine code 1NZ (1490 cc) vs 2ZR (1790 cc)
Ipi nzuri kwa yafuatayo
1. Ulaji wa mafuta
2. Uimara/kudumu
3. Upatikanaji wa spare
4. Uwezo wa kuchanganya speed mfano kutoka 20 ->120 KPH in few seconds
 
huwez sema mark 2 ya zamani ina 1G kavu ...mark au gari zingne zina injini nyingi ( option) mfano kwenye mark 2 ya 98 ina ijz gte sasa ww sijui unasema ipi !!
Mark 2 ya zamani nyingi zina 1G kavu hiyo 1jz inafungwa kwenye toyota aristo
 
Osaba itakuwa engine na magari yake huyajui !! toyota ukiwauliza 1jz imefungwa wap watakupa list zao ambapo verosa vr25 lazima iwepo mark 2 nk ni sawa na ww unavyojua 1g kwa mark 2 mi naijua kwa alteza na crown nk....mark 2 haikuumbiwa 1G
 
Back
Top Bottom