Supplemental Restraint system (SRS- Airbag) warning light...
Kwa upande wangu nasema hiyo si warning light bali ni DANGEROUS LIGHT.....Never take it for granted..
Taa ya onyo inawaka njano au orange na Taa ya HATARI inawaka nyekundu..
Hiyo taa inapowaka inaashiria mfumo mmojawapo wa SRS airbag haufanyi kazi....imaweza kuwa fuse mbovu au hata computer inyohusika na SRS Airbag au kitu kingine chochote kinachounda mfumo wa SRS Airbag.
Madhara ya kuwaka kwa hiyo taa ni kupelekea kutokufunguka kwa Airbags pale utakapopata ajali......hivyo madhara ya ajali yatakuwa makubwa zaidi kiasi kwamba ajali ambayo ulikuwa u-survive kwa msaada wa SRA Airbag, basi bila SRS Airbag mhanga wa ajali hiyo atapoteza maisha..
Hatua za awali kagua fuse ya SRS Airbag kama ni nzima au imeungua....kama ni nzima nenda kafanye diagnosis ili upate code inayohusika na eneo linalosumbua....
Endapo utakuta fuse imeungua, jiulize ni kwa nini imeungua....huenda kuna short circuit kwenye mfumo mzima wa SRS Airbag.
Taa hiyo ikiwaka na gari ikapata ajali, abiria na dereva wanaumia sawa tu na mtu aliyeko ndani ya bajaji..
NB.....kuna baadhi ya model za magari seat belt inaunganishwa na SRS Airbag module hivyo usipofunga mkanda, SRS Airbag haita operate vizuri wakati wa impact ya ajali..
Kwa gari lako sijajua kama lipo hivyo ila kama ukifunga mkanda , taa bado inawaka, wahi kwa fundi ufanye vipimo..
Sent using
Jamii Forums mobile app