Naomba kujua jinsi ya kuandaa ndizi aina ya Mkono wa Tembo

Naomba kujua jinsi ya kuandaa ndizi aina ya Mkono wa Tembo

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Nimekata hizi ndizi kubwa kubwa Sana, hapa kwetu zinaitwa mkono wa tembo, sijawahi kuzila hata siku moja.

Naomba wataalamu wabobezi wa Aina mbalimbali ya kuziandaa ndizi hizi kwa ajili ya kula mnielimishe namna ya kuziandaa.

Nimetumia neno kuandaa kwa sababu Kuna Aina mbalimbali ya kuzipika ama kuzikaanga ama kuzichoma.

Kwa kweli sijui,naomba mnipe elimu hapa.
 
Katakata pika kama mzuzu tu hazina tofauti, ukitaka weka nazi ila bibi alikua anaweka maziwa na Maharage mabichi labda kambare au kitimoto tamu balaa.
 
Zi - roast ule na kachumbari au kifungwa kinywa. Hazifai kupika!
 
Unaziacha kwanza zikikaribia kuiva unazirost, ni tamu balaaa
 
Awali mkono wa tembo nilikuwa naziacha ziive kidogo then nazirost kwenye mafuta nanywea chai.

Siku hizi ninapenda kuzipika kama chakula,naziacha ziive(siziwe tepetepe),nakaanga kitunguu,naweka nyanya kiasi,zikiiva naweka ndizi ambazo nimeshazikata..zikikaribia kuiva naweka hoho, karoti, iriki na tui la nazi,then naziacha kidogo huku nikiangalia tui lisikatike.Unaweza weka maziwa fresh badala ya tui nazi.Ni tamu sana sana pembeni ukiwa umerost nyama/maini/kuku yako unaweka kwa sahani
 
Huku Tanga zinachemshwa zinatiwa iliki na nazi..mara nyingi zile zilizoiva.
 
Back
Top Bottom