Awali mkono wa tembo nilikuwa naziacha ziive kidogo then nazirost kwenye mafuta nanywea chai.
Siku hizi ninapenda kuzipika kama chakula,naziacha ziive(siziwe tepetepe),nakaanga kitunguu,naweka nyanya kiasi,zikiiva naweka ndizi ambazo nimeshazikata..zikikaribia kuiva naweka hoho, karoti, iriki na tui la nazi,then naziacha kidogo huku nikiangalia tui lisikatike.Unaweza weka maziwa fresh badala ya tui nazi.Ni tamu sana sana pembeni ukiwa umerost nyama/maini/kuku yako unaweka kwa sahani