Sheria ya uraia inasema wazi kabisa kua "hili mtu awe mtanzania basi inatakiwa wakati anazaliwa mmoja wa au wazazi wake wote wawili walikua ni watanzania" ni wakati wa kuzaliwa, kama mtoto wakati anazaliwa hapa Tanzania na wazazi ambao kwa wakati huo hawakua waTanzania basi automatically mtoto huyu sio mTanzania ila tu ata pata haki yake ya uTanzania pasipo kujali uraia wa wazazi wake akifikisha miaka 18 na kuukana uraia wa wazazi wake na hapa anakua na advantage kama raia wa kuzaliwa.
Endapo alitoka nje ya nchi, na hapa kunacontradiction sasa alitumia passport ya nchi gan sasa kusafiria ilihali ni stateless? Ila anyway kama aliondoka kwenda kusoma na huku nyuma wazazi wake wakakamilisha taratibu za uraia na wakawa raia basi huyu mtoto bado akirudi hawezi kua raia nae mpaka afuate taratibu zile nilizo sema za kuukana uraia wa wazazi wake na wake wa awali wowote na hawezi kupata uraia wa kurithi automatically sababu wakati wazazi wake wanapewa uraia yeye alikua kashazaliwa na muda wanapewa alikua tayari ana uelewa wa mambo.