Naomba kujua kama mwimbaji nguli wa kike wa Koffi Olomide Cindy le cour kama amehama bendi

murume

Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
90
Reaction score
80
Nijuzeni kama kweli Cindy le cour kaachana na bendi ya koffi olomide
 
Sina uhakika, naamin bado yupo na Koffi maana pale kapewa nafasi kubwa ya kuonyesha kipaji chake kuliko kokote anakoweza kwenda.

Kama unapenda stori za hivyo check congovibes.com. Huko utakutana na stori za Argos ambaye huongea mara kwa mara na wanamuziki wakubwa wa Congo.
 
Inawezekana kama koffi karudisha majeshi kwa mama watoto wake aaliyah
 
Ila yule Cindy jamani ana sauti nzuri. Ukipata nafasi sikiliza sauti yake kwenye wimbo wa molounge, ikea, desormaise ba je taime bila kusahau skol mandra mada.
 
Ila yule Cindy jamani ana sauti nzuri. Ukipata nafasi sikiliza sauti yake kwenye wimbo wa molounge, ikea, desormaise na je taime bila kusahau skol mandra mada.
 
Hivi bado kuna watu mnasikiliza nyimbo za Koffi!!! Ni pm nikutupie vibao balaa vya Ferre Gola alivyotoa mwaka huu akipewa shavu na vijana wake Chikito na Fabrigas. Huwa nikivisikiliza najikuta nasinzia hata kazini kwa namna jamaa anavyolalamika kwa sauti nzito baadae anailainisha kwa ustadi usio na kipimo .
 

Mapenzi na mahaba kaka.
 
Mapenzi na mahaba kaka.

Kweli kaka. Lakini siku ukiweka pembeni ushabiki ukaamua kuchuja mwanamziki anayekonga nyoyo basi ni Ferre Gola. Hebu download wimbo "Biberon" usikilize hadi mwisho utaniambia jamaa alivyo nuksi.
 
Naunga mkono mapenzi ni mahaba. Miye huniambii kitu kwa Koffi. Nasikitika amesema anatoa albamu ya mwisho.
 

Wewe jamaa ujasiri wa kumkandia le grand mopao unautoa wapi?? Hebu tafakari halafu uje kuomba msamaha hapa!!..mopao hakosolewi..mopao muasisi wa rhumba za kisasa hakosolewi mzee
 
Kwanza fabrigas hajawahi kuimba kwa bendi ya ferre gola kwani alitokea kwa werrason na kwa sasa anamiliki bendi yake ila chikito ameshaondoka kwa ferre gola pamoja na kina rkelly na nicodemus ambao wameenda kwa werrason ila ndio ferre gola anaimba lakini huwezi kumfananisha na koffi kwani koffi anamchango mkubwa sana kwenye mziki wa kikongo na mziki anaufahamu kweli
 

Hao kina derre na falli wote walikua wanenguaji kwa kofi na ujuzi wa kuimba wamepata pale..sasa mtu anaposema kofi hamna kitu huyo hajui mziki...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…