Hili linchi bwana sijui lilipataga laana ama!!! Kwanini ushuru wa magari upo juu sana na haushuki!! Ukinunua gari nje, ulizia ushuru wake utashika kichwa kama sio sawa na kununua gari la pili ama mawili kama hilo hilo dahh[emoji33][emoji33]
Ningeishauri serikali washushe ushuru wa magari n.k ili watu wasiishi na magari mabovu, mtu anaona bora anunulie hapa kuliko kuagiza nje, na magari ya hapa kama munavyojua ni chakavu sana. Serikali tuhurumieni, mama Samia najua wewe ni mama mwenye huruma na imani, nakuomba ulifanyie kazi suala hili.