Cheque/ Hundi zipo za aina mbili kama ulivyozitaja hapo juu isipokua hiyo moja inaitwa crossed cheque.
1. Open cheque, inaandikwa jina la mlipwaji binafsi na sio kampuni, shirika au kikundi. Hii ukipewa unaenda benki husika ya aliyekuandikia cheque unapewa pesa hapo hapo dirishani.
2. Crossed cheque, hii inaweza kulipwa kwa mtu au kampuni. Tofauti yake ni kwamba, haupewi pesa mkononi, unatakiwa uiweke kwenye akaunt ya benki yako. Hapo itachukua takriban siku mbili ili uweze kuipata pesa yako.
Pia siku hizi malipo ya hizi cheque hazizidi 10 M.
Baadhi ya benki kama sio zote siku hizi hata ukilipwa open cheque wanasumbua kulipa, wanasema uwe na akaunt nao au aliyekulipa akutambulishe kwao. Huu ni usumbufu na kinyume cha taratibu. Huenda wizi na udanganyifu umepelekea hii hatua. Wanasema hawalipi third party.