jaffari odhiambo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 526
- 13
Katika mahakama ya wilaya ya Bunda -Mara kuna wafanyakazi wanaoitwa makarani. Sasa ukienda pale ili ujaziwe fomu halafu usainiwe na mh. Hakimu unaombwa hela ati hakimu hawezi kusaini bila hela. Je, huo ndio utaratibu ama ni rushwa ya kijanja janja? Naomba kueleweshwa maana sijui kama ndio utaratibu wa mahakama hizi zetu za TANZANIA ama ni utaratibu wa pale BUNDA tu ama namna gani. Mnifahamishe jamani wanajamvi wenzangu. Hela yenyewe ni sh.5000 tu ya kitanzania.