Adolph
JF-Expert Member
- Sep 26, 2010
- 895
- 346
Wakuu nianze na salam
Nina mtaji wangu wa tsh 7,000,000/= na eneo ninalokaa hakuna gym yoyote na watu wenye uhitaji wa gym ni wengi mno...ningependa nianzishe gym centre ila tatizo sina uzoefu hata kidogo na hii biashara..
Ningependa kuomba ushauri wenu je kwa mtaji huo naweza kuanzisha gym ?
Je kwa mtaji huo naweza kuanzisha gym itayokuwa angalau na sifa za gym?
Je ni vitu gani vya muhimu vya kuzingatia na wapi nitakaponunua vifaa kwa bei nafuu?....
Ningependa gym iweze ku-accommodate watu 10 kwa wakati mmoja.. Kuhusu suala la eneo halina shida maana ukumbi upo.
Naombeni ushauri wenu wadau
================================================
MASWALI MENGINE KUHUSU BIASHARA HII
================================================
============================================
MAJIBU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI

Habari zenu wapendwa jamani mie nimekuwa na wazo la kuanzisha gym, naombeni mawazo yenu maana sio mzoefu sana na mambo hayo ila naona ni business nzuri, tatizo nilitaka kujuaa ni upatikanaji wa vifaa, eneo la biashara hiyo na changamoto mbalimbali naomba michango yenu jamani, na hata mtaji natakiwa nianzie na mtaji wa kiasi gani. asanteni
Ninahitaji kuanzisha Gym ndogo ya kawaida tu je kwa manunuzi ya vifaa tu nahitajika kuwa na sh. Ngapi??
============================================
MAJIBU KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI
============================================
Mimi binafsi kama ningelikuwa ni wewe kitu cha kwanza kabla sijaanza kuufikiria huo mradi ningemtafuta lawyer aliyebobea ktk sheria za michezo na wanamichezo pamoja na biashara za michezo,biashara ya Gym ina regulations nyingi sana ambazo nyingi zake zitakula noti yako sana,mimi nina rafiki mmoja ninajaribu kumpata hivi sasa ambaye baba yake ndio watu wa kwanza kuanza hiyo biashara hapa nchini nafikiri kama umewahi kumsikia ni maarufu sana hususani ktkruninga anaitwa mzee Hamza Kassongo huyu mzee mtoto wake mkubwa ni rafiki yangu nilikuwa nacheza naye kabumbu Dar zamani nakuahidi siku akipatikana nitakujuza habari zote nitakazopata tokea kwake kuhusu hiyo biashara unayotaka kujihusisha nayo.Usikate tamaa ndugu yangu hapa ni mahali pazuri unaweza ukapata msaada kuhusu swali lako.M/Mpamba.
Mtaji wa kwanza Baunsa, utakuwa unamlipa kama mwalimu 300,000/month kwa mwaka 3.6mil na pesa ys kula kila siku. Unahitaji kukodi jengo tena lenye nafadi ya kutosha kwa ajili ya maxoezi mbalimbali 500,000/= per months kwa mwaka 7.2mil, vifaa vile basic yani vyuma, smith machine, bench, baskelu, kamba vitakugarimu milioni 15. Radio na tv 0.5 mil. Jumla ni kama mil 27 inatosha kama mtaji