Hii kwa mujibu wa kamusi ya TUKI kuwa "sorry" ni "samahani"
View attachment 1256098
Vile vile kwa mujibu wa google translate neno "sorry" ni "samahani"
View attachment 1256100
Nilichokuwa nakieleza nimerejea tafsiri ya kimazingira na sio tafsiri ya neno kwa neno na ndio maana nikaeleza kuwa neno "sorry" linaweza kuwa na maana ya samahani au pole vile vile ukiangalia samahani(nomino) na samahani(kitenzi) haibaki vile vile kuwa "sorry" na pia tukumbuke urasmi wa lugha hauzuii usahihi wa lugha mwisho pia nakubaliana na wewe kuwa inawezekana kiswahili kikawa na msamiati michache na ndio maana tafsiri ya kimazingira huwa naitumia zaidi.
Ni ukweli upo sahihi 😬Msamaha= nomino, samehe= kitenzi, samahani= kielezi.
Bado Sorry haiwezi kuwa na maana ya samahani, kama ni hivyo Excuse ina maana gani??, je mahali pa Excuse unaweza kuweka sorry??.
Tusishikilie makosa ya kimazoea na kuyahalalisha, (justification of common mistake in language.)🤣🤣