Naomba kujua namna ya kupika kande kwa mahindi mabichi

Naomba kujua namna ya kupika kande kwa mahindi mabichi

k-bee

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2017
Posts
966
Reaction score
1,084
Rejea mada tajwa hapo juu,

Naomba kujuzwa namna ya kupika kande mahindi mabichi kwa maharage makavu na kama kuna viungo na vikorombwezo vya kuweka ili yawe na ladha murua.

Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Osha na Kisha bandika maharage yako jikoni...Chukua mhindi wako kisha Anza kupukuchua (kutenganisha mahindi na gunzi)..maharage yakikaribia kuiva changanya na mahindi yako yaliyosafishwa vizuri....ongeza chumvi na subiria kuiva.upande mwingine kaanga kitungua kwenye mafuta kidogo Kisha ongeza nyanya zikiiva waweza kuweka Nazi au karanga au mtindi, vikichemka ongeza kwenye mahindi yako Kisha subiria mpaka vichemke na kuchanganyikana vizuri halafu ipua na hapo kiko tayari kwa ajli ya kuliwa. Waweza kuongeza pilipili hoho, manjano, binzari kitunguu swaumu n.k ktk pishi lako.kila la kheri
 
Back
Top Bottom