Osha na Kisha bandika maharage yako jikoni...Chukua mhindi wako kisha Anza kupukuchua (kutenganisha mahindi na gunzi)..maharage yakikaribia kuiva changanya na mahindi yako yaliyosafishwa vizuri....ongeza chumvi na subiria kuiva.upande mwingine kaanga kitungua kwenye mafuta kidogo Kisha ongeza nyanya zikiiva waweza kuweka Nazi au karanga au mtindi, vikichemka ongeza kwenye mahindi yako Kisha subiria mpaka vichemke na kuchanganyikana vizuri halafu ipua na hapo kiko tayari kwa ajli ya kuliwa. Waweza kuongeza pilipili hoho, manjano, binzari kitunguu swaumu n.k ktk pishi lako.kila la kheri